MABONDIA watano waliopigana na mabondia wote Floyd Mayweather na Manny Pacquiao ambao watakutana ulingoni kesho ukumbi wa MGM Grand mjini Las Vegas, wametoa maoni yao juu ya wawili.
Na kwa ujumla Pacquiao anatajwa kuwa bondia hatari zaidi ulingoni kuliko mpinzani wake Mayweather, lakini Mfilipino huyo anapigika tofauti na mpinzani wake huyo wa Marekani. Endelea.
OSCAR DE LA HOYA; Aliyepigwa kwa pointi na Mayweather mwaka 2007 na akapigwa kwa Technical Knockout (TKO) na Pacquiao raundi ya nane mwaka 2008, anasema; "Nampa nafasi ya kushinda Pacquiao,".
Floyd Mayweather alimshinda kwa pointi Oscar de la Hoya
Sura ya De La Hoya baada ya pambano na Mayweather (kushoto) na kulia baada ya pambano na Pacquiao
RICKY HATTON; Aliyepigwa na Mayweather kwa TKO raundi ya 10, mwaka 2007 na akapigwa kwa Pacquiao kwa Knockou (KO) raundi ya pili mwaka 2009 anasema; "Bado narudia kuelea hisia zangu za awali, Floyd atafanyia kazi namna ya kumpiga (Pacquiao),".
Hatton baada yaa pambano na Mayweather (kushoto) na kulia baada ya pambano na Pacquiao
JUAN MANUEL MARQUEZ; Aliyepigwa kwa pointi na Mayweather mwaka 2009, akatoa sare na
Pacquiao mwaka 2004. Akampiga Pacquiao kwa pointi mwaka 2008. Akapigwa na Pacquiao kwa pointi mwaka 2011. Akampiga Pacquiao kwa KO raundi ya sita mwaka 2012. Marquez anasema; "Mayweather ana staili nzuri ya kushinda hili pambano. Ikiwa Manny atashinda, itakuwa nzuri kwangu. Moyo wangu upo kwa Pacquiao [lakini] nafikiri Mayweather ni bora zaidi ya Pacquiao.'
Marquez alimpa matatizo Pacquiao katika mapambano yote manne waliyokutana. Hapa Pac Man amelala 'usingizi mnono' baada ya kupewa kitu na mbabe wake huyo
SHANE MOSLEY; Aliyepigwa na Mayweather kwa pointi mwaka 2010 na akapigwa kwa pointi pia na Pacquiao mwaka 2011 anasema; "Nilimpa wakati mgumu Mayweather, lakini akashinda. Floyd atashinda.'
Mosley baada ya pambano na Mayweather kushoto na kulia baada ya pambano na Pacquiao
MIGUEL COTTO; Aliyepigwa kwa pointi na Mayweather mwaka 2012 na akapigwa na Pacquiao kwa TKO raundi ya 12, mwaka 2009 anasema; "Manny ana kasi, nguvu na Freddie katika kona yake. Nampa PacMan.'
Cotto kushoto baada ya pambano na Mayweather na kuliwa akiwa 'amelowa' damu baada ya pambano na Pacquaio
PICHA ZAIDI NENDA:
http://www.dailymail.co.uk/sport/boxing/article-3063123/Floyd-Mayweather-Manny-Pacquiao-fought-five-opponents-came-top.html#ixzz3YtSjRDPK
0 comments:
Post a Comment