MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Daniel Sturridge amekwenda kumuona mtaalamu mjini Boston, Marekani ili kujua kama atahitaji upasuaji kutatua tatizo lake la paja.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa England amecheza mara mbili tu tangu aumie katika mechi dhidi ya Manchester United Machi 22 na kocha Brendan Rodgers wiki iliyopita alielezea wasiwasi wake kama mshambuliaji huyo atacheza tena msimu huu.
Sasa hali inaelekea kuwa hivyo, baada ya Sturridge kwenda kumuona Dk Peter Asnis kujua mustakabali wa maumivunyake.
Daniel Sturridge amekwenda Marekani kujua kama atahitaji upasuaji wa paja lake
Sturridge pia aliwahi kwenda Los Angeles, Marekani kufanya mazoezi ya kutafuta nafuu ya maumivu yake
Hii ni mara ya pili kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, Sturridge anapelekwa Marekani kwa sababu ya maumivu yake.
Desemba mwaka jana alikuwa Los Angeles na baadaye Boston kujifua kutafuta ahueni ya maumivu hayo yaliyomuweka nje kwa miezi mitano.
Rodgers sasa atalazimika kutoa fedha kununua mshambuliaji mwingine kwa ajili ya msmu ujao, kutokana na matatizo ya Sturridge. Nyota wa PSV Eindhoven, Memphis Depay ndiye mlengwa wake wa kwanza na mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uholanzi inasemekana yuko tayari kuhamia Anfield.
0 comments:
Post a Comment