KLABU ya Liverpool itakuwa na mazungumzo mazito na winga wake, Raheem Sterling wiki hii baada ya mchezaji huyo kumtamkia kocha Brendan Rodgers anataka kuondoka.
Sterling alifanya maungumzo binafsi na Rodgers kabla ya mechi iliyoisha kwa sare ya 1-1 dhidi ya Chelsea na akaweka wazi hataki kubaki Anfield.
Lakini mwanasoka huyo wa kimataifa wa England akakubali kukutana na klabu kwa mazungumzo ya mwisho kabla ya kufanya uamuzi rasmi wa kubaki, au kuondoka Merseyside.
Raheem Sterling (pichani) anaweza kuondoka LIverpool baada ya Ligi
Sterling hana furaha Liverpool na amemuambia Brendan Rodgers anataka kuondoka PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Sterling amegoma kusaini Mkataba mpya wa miaka mitano kwa sababu haridhishwi na uwezo wa timu kiushindani, kwani kiu yake ni kucheza Ligi ya Mabingwa na kushinda mataji.
Aidha, mshahara wa Pauni 90,000 kwa wiki anaolipwa sasa haumridhishi, ingawa klabu imeahidi kumpandishia hadi 100,000 katika mkataba mpya.
Vigogo wote wa Nne Bora Ligi Kuu England, kuanzia mabingwa Chelsea, Manchester City, Arsenal na Manchester United wanamtaka kinda hiyo na wamekuwa wakimfuatila kwa karibu.
Real Madrid ya Hispania, Bayern Munich ya Ujerumani na Juventus ya Italia pia inataka huduma za mchezaji mwenye umri wa miaka 20.
0 comments:
Post a Comment