SEVILLA ya Hispania imefanikiwa kutetea Kombe la Europa League baada ya kutoka nyuma na kushinda mabao 3-2 dhidi ya Dnipro usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa fainali uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Warsaw. Poland.
Nikola Kalinic alianza kuifungia Dnipro dakika ya saba, kabla ya Sevilla kuzinduka na kupata mabao mawili ya haraka kupitia kwa Grzegorz Krychowiak na Carlos Bacca ndani ya dakika tatu.
Nahodha wa Dnipro, Ruslan Rotan akaifungia timu hiyo ya Ukraine bao la kusawazisha kwa shuti la mpira wa adhabu kaba ya mapumziko na Bacca akafunga bao lake la pili katika mchezo huo na la ushindi kwa Sevilla dakika ya 73.
Kwa matokeo hayo, Sevilla itacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kutetea taji la Europa League. Beki wa Dnipro, Matheus alipoteza fahamu baada ya kugongana kichwani na Benoit Tremoulinas.
Kikosi cha Sevilla kilikuwa; Rico, Vidal, Kolodzjejczak, Carrico, Tremoulinas, Krychowiak, Mbia, Banega/Iborra dk87, Reyes/Coke dk58, Vitolo, Bacca/Gameiro dk82.
Dnipro; Boyko, Fedetskyi, Douglas, Cheberyachko, Leo Matos, Kankva/Shakhov dk85, Fedorchuk/Bezus dk68, Matheus, Rotan, Konoplyanka na Kalinic/Seleznyov dk78.
Wachezaji wa Sevilla wakisherehekea na Kombe la Europa League jana Uwanja wa Taifa wa Warsaw, Poland PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment