MSHAMBULIAJI Raheem Sterling amepata mapokezi mazuri katika usiku wa tuzo za Liverpool usiku huu ukumbi Echo Arena wakati anatajwa Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa klabu hiyo.
Saa kadhaa baada ya kuelezwa amemuambia kocha Brendan Rodgers anataka kuondoka Anfield, kinda huyo wa umri wa miaka 20 aling'ara tena akipokea tuzo yake katikati ya Jiji.
Wakati anatoa hotuba fupi ya kushukuru kelele za 'Baki Raheem' zilitawala ukumbini, lakini alipomaliza na kuondoka walisikika baadhi ya watu kati ya mashabiki 3,000 wakizomea.
Raheem Sterling ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka Liverpool usiku huu ukumbi wa Echo Arena PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Wakati alipotajwa katika video iliyokuwapo ukumbini hapo kwamba anakwenda kuchukua tuzo, wengi walimshangilia.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 alipanda basi moja na wachezaji wenzake wote jioni ya leo kutoka makao makuu ya Liverpool, Melwood kwenda ukumbi wa Echo Arena kwenye sherehe hizo.
Sterling alionekana akiwasili viwanja vya mazoezi na Range Rover yake nyeupe mchana kabla ya kupanda basi la wachezaji wakiwa wamevalia suti nyeusi nadhifu.
0 comments:
Post a Comment