MSHAMBULIAJI wa PSV, Memphis Depay amethibitishwa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uholanzi, maarufu kama Eredivisie baada ya mechi za mwisho za ligi hiyo Jumapili.
Kinda huyo wa umri wa miaka 21, ambaye amekubali kujiunga na Manchester United msimu ujao kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 25, amefunga mabao 22 katika mechi 30 alizocheza, na kuwa mchezaji mdogo zaidi kutwaa tuzo hiyo tangu mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Ronaldo mwaka 1995.
Depay amekuwa na mchango mkubwa kwa PSV kutwaa taji la ligi ya Uholanzi msimu huu, kikosi cha kocha Phillip Cocu kikiwazidi kwa pointi 17 Ajax walioshika nafasi ya pili. Walimalizia msimu kwa ushindi wa 3-2 ugenini dhidi ya ADO Den Haag.
Mshambuliaji wa PSV, Memphis Depay ametwaa tuzo ya ufungaji bora Eredivisie msimu wa 2014-2015 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment