TIMU ya taifa ya Namibia imetinga Robo Fainali za michuano ya Kombe la COSAFA 2015 baada ya kuifumua mabao 4-1 Zimbabwe katika mchezo wa mwisho wa Kundi A Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini usiku huu.
Ushindi huo, unaifanya Namibia kuongoza Kundi mbele ya Zimbabwe, ambayo kwa kumaliza nafasi ya pili inarejea nyumbani.
Namibia sasa itakutana na mabingw awatetezi, Zambia katika Uwanja huo huo Jumapili kuanzia Saa 9:00 Alasiri.
Mabao ya Namibia yalifungwa na Chris Katjiukua, Deon Hotto mawili na Sadney Urikhob, wakati la kufutia machozi la Zimbabwe limefungwa na Raphael Manuvire kwa penalti.
Katika mchezio mwingine wa Kundi A leo, Mauritius imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Shelisheli, bao pekee la Jean-Pierre Sophie.
Mauritians imemaliza nafasi ya tatu katika kundi hilo na kesho mechi za Kundi B zitahitimishwa Madagascar ikimenyana na Swaziland Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace kuwania Robo Fainali.
Madagascar itahitaji sare tu ili ifuzu kwa wastani mzuri wa mabao, wakati Swaziland ni lazima ishinde ili kutimiza ndoto za kwenda Robo Fainali. Tanzania itamenyana na Lesotho kuwania nafasi ya tatu ya kulinda heshima zirejee nyumbani japo na tabasamu, baada ya timu zote hizo kufungwa mechi zoite mbili za mwanzo.
0 comments:
Post a Comment