KWA mara ya kwanza baada ya miaka mingi, ukumbi wa Mango Garden Kinondoni unapitisha wikiendi bila burudani yoyote na badala yake onyesho la Yamoto Band na Mashauzi Classic leo usiku ndio show pekee wiki hii katika ukumbi huo.
Twanga Pepeta ambao hupiga Mango Garden kila Jumamosi, Jumamosi hii watakuwa Wenge Garden Ukonga.
Bendi ya FM Academia ambayo huibuka Mango Garden na kufukia viraka vya bendi zilizopata dharura ya kuhama ukumbi, Ijumaa hii itakuwa Polisi Kilwa Road wakati Jumamosi itakuwa Leaders Club katika tamasha la nyama choma.
Yamoto Band watakwea jukwaa la Mango Garden Kinondoni leo usiku (Alhamisi, 28) kuonyeshana kazi na wenyeji wao Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi.
Ni onyesho ambalo limeteka hisia za mashabiki wa muziki kutokana na ukweli kuwa vikundi hivyo viwili havijawahi kukutana katika katika onyesho la pamoja, ukiondoa yale matamasha yanayoshirikisha wasanii wengi.
0 comments:
Post a Comment