KLABU ya Liverpool imefuta mpango wa kufanya mazungumzo na washauri wa Raheem Sterling yaliyotarajiwa kufanyika kesho, kufuatia wakala wake 'kusema mbovu'.
Katika gazeti la London Evening Standard, Aidy Ward amesema Sterling hatasaini Mkataba mpya Liverpool hata apewe ofa ya mshahara wa Pauni 700, 000, 800,000 au 900,000 kwa wiki, hivyo kwa maana hiyo, Liverpool imeona hakuna sababu ya mazungumzo.
Ward amekuwa akisistiza msimamo wake wiki yote hii, kabla ya kuweka wazi usiku wa Jumatatu kwamba kikao kilichoandaliwa na viongozi wa Liverpool kitaishia kwa Sterling kusema anataka kuondoka.
Sterling kulia akiwa na tuzo yake ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka Liverpool na kushoto ni wakala wake, Ward
Liverpool imempa ofa ya mshahara wa Pauni 100,00 Sterling kwa wiki katika Mkataba mpya anaotakiwa kusaini ambao aliukataa February na mazungumzo baina ya pande hizo mbili yakapangwa kufanyika mwishoni mwa msimu.
Mwanasoka huyo chipukizi wa kimataifa wa England alitarajiwa kuhudhiria na Ward.
Sterling na Ward walitarajiwa kukutana na kocha Brendan Rodgers na Mtendaji Mkuu Ian Ayre mjini Liverpool kesho katika viwanja vya mazoezi vya Melwood.
Lakini Liverpool imeamua haitafanya tena mkutano huo, baada ya Ward kuweka wazi msimamo wake.
Ward anatarajia Manchester City au Chelsea kuwa klabu mpya ya Sterling, huku akikataa mpango wa kumpeleka kijana wake Real Madrid, Barcelona au Bayern Munich.
0 comments:
Post a Comment