DEREVA wa mbio za magari, Lewis Hamilton amemaliza utata wa Mkataba na kampuni ya Mercedes, baada ya kusaini Mkataba mpya wa miaka mitatu wenye thamani ya Pauni Milioni 100.
Mercedes imetoa habari kwamba dereva huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye Mkataba wa sasa ilikuwa umalizike mwishoni mwa msimu, atabakia katika timu hiyo kuelekea mbio za Monaco Grand Prix mwishoni mwa wiki.
Hamilton amesaini Mkataba wa miaka mitatu ambao utamuweka katika timu hiyo ya Uingereza hadi mwaka 2018. Bingwa huyo mara mbili mfululizo wa dunia pia anakuwa mwanamichezo wa Uingereza anayelipwa zaidi.
Lewis Hamilton akisaini Mkataba mpya na mabingwa wa dunia, Mercedes PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Hamilton aliyejiunga na Mercedes mwaka 2003, ambaye atakuwa mwanamichezo anayelipwa zaidi Uingereza, alikuwa mwenye furaha mjini Monaco leo na akasema; "Mercedes ni nyumbani kwangu na nitakuwa mwenye furaha kubaki hapa kwa miaka mingine mitatu," amesema Hamilton, ambaye alimshinda mchezaji mwenzake wa timu ya Mercedes, Nico Rosberg katika michuano ya dunia kwa pointi 20.
Pato lake kwa mwaka litakuwa Pauni 33,333,333, kwa wiki Pauni 641,026, kwa siku Pauni 91, 575 kwa mbio moja Pauni 1,571,429 katika mbio 21 za msimu.
0 comments:
Post a Comment