Na Prince Akbar, SOUSSE
DEO Munishi ‘Dida’ anaanza katika lango la Yanga SC dhidi ya Etoile du Sahel usiku wa leo nchini Tunisia.
Kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm atamuanzisha kipa huyo badala ya Ally Mustafa ‘Barthez’ aliyedaka mechi ya kwanza mjini Dar es Salaam, Yanga.
Dida atalindwa na Juma Abdul kulia, Oscar Joshua kushoto na Mbuyu Twite na Kevin Yondan katikati. Viungo ni Said Juma, Salum Telela na Mrisho Ngassa wakati washambuliaji ni Simon Msuva, Amissi Tambwe na Kpah Sherman.
Yanga watakuwa wageni wa Etoile du Sahel Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse, Tunisia katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga SC waliofika juzi usiku Tunisia, wanahitaji ushindi wa ugenini au sare ya kuanzia mabao 2-2 ili kusonga mbele, baada ya awali kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani Dar es Salaam.
Sare nyingine ya 1-1 itaurefusha mchezo huo hadi kwenye dakika 120 ambako pia mshindi asipopatikana mikwaju ya penalti itatumika.
Refa Mganda, Dennis Batte aliyefupisha safari ya Tanzania katika mbio za Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2015 Equatorial Guinea, ndiye atachezesha mchezo huo leo.
Batte atasaidiwa na Waganda wenzake, Mark Ssonko na Balikoowa Musa Ngobi, ambao watakuwa washika vibendera.
Batte ‘aliiuma’ Taifa Stars wazi wazi ikifungwa mabao 2-1 na wenyeji Msumbiji Agosti 3, mwaka jana Uwanja wa Zimpeto mjini Maputo katika mchezo wa marudiano, hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza fainali hizo ambazo awali ilikuwa zipigwe Morocco.
Televisheni namba moja Tanzania ya michezo na burudani- Azam TV itaonyesha moja kwa moja mechi hiyo kutoka Tunisia kuanzia Saa 1:00 usiku kwa Saa za Kaskazini mwa Afrika na Saa 3:00 usiku kwa Saa za Afrika Mashariki.
Etoile du Sahel wamethibitisha kufikia makubaliano na Azam TV kurusha mchezo huo ‘Live’ leo. Kila la heri Yanga SC.

0 comments:
Post a Comment