WINGA Memphis Depay amepigwa pichwa akiondoka viwanja vya mazoezi vya Manchester United vya Aon baada ya kufanyiwa vipimo vya afya jana.
Mholanzi huyo anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na United kwa ajili ya msimu ujao na aliwasili maskani yake mpya jana kwa ajili ya taratibu za kukamilisha uhamisho wake.
Depay alitua Manchester, kabla ya kwenda kwenye viwanja vya mazoezi vya Aon kwa ajili ya vipimo vya afya, na alipigwa picha akiondoka eneo hilo jana mchana akiendeshwa na Ofisa wa United.
Memphis Depay (nyuma) akiondoka viwanja vya mazoezi vya Manchester United, Aon baada ya kukamilisha vipimo vya afya PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Baadaye klabu hiyo ikatweet kwamba Depay amekamilisha vipimo vyake vya afya, na United sasa itasonga mbele kukamilisha usajili wake wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa Juni.
Kinda huyo wa umri wa miaka 21- atajiunga na United baada ya msimu mzuri wa mafanikio ligi ya Uholanzi, maarufu kama Eredivisie, akiiwezesha PSV Eindhoven kuwa bingwa kwa mabao 22 katika mechi 30 yaliyomfanya awe mfungaji bora wa timu.
0 comments:
Post a Comment