David de Gea (katikat) akiwasili katika tuzo za kufungia nsimu za Manchester United pamoja na mchezaji mwenzake, Juan Mata PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KIPA David de Gea anayetajwa kutaka kuhamia Real Madrid ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Manchester United usiku wa jana.
Na baada ya kupewa tuzo hiyo, kipa huyo wa zamani wa Atletico Madrid, ambaye Mkataba wake unamalizika mwakani, alisema: "Nataka kusema asanteni kwa wachezaji wenzangu, wamekuwa babu kubwa msimu huu na ninafikiri tuna chumba kizuri cha kubadilishia nguo. Nawapenda,".
Mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Hispania, De Gea- Juan Mata ameshinda tuzo ya Bao Bora la Msimu alilofunga katika mechi dhidi ya Liverpool.
0 comments:
Post a Comment