KIUNGO Mbrazil, Philippe Coutinho ametamba kwenye tuzo za Liverpool akibeba hadi tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Liverpool.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 tu amethibitishwa kushinda tuzo hiyo inayotokana na kura za mashabiki katika hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika usiku wa jana ukumbi wa ECHO Arena.
Coutinho amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu mgumu kwa Liverpool, tena akiifungia timu mabao muhimu.
Mabao ya mashuti la mbali dhidi ya Bolton Wanderers katika mchezo wa Kombe la FA na Southampton katika Ligi Kuu ya England yakiwa miongoni mwa mabao yake ya kukumbukwa msimu huu pamoja na la ushindi dhidi ya Manchester City Uwanja wa Anfield.
Ameifungia timu ya Brendan Rodgers mabao manane katika mashindano yote msimu huu na kwa hakika amewavuia wengi kwa soka yake.
Rodgers alisema mapema kwamba Coutinho ana nafasi nzuri ya kuziba pengo la Luis Suarez aliyetimkia Barcelona msimu uliopita.
"Unaweza kulipa fedha zako kumuangali huyu kijana," Rodgers alisema February. "Ni mfano wa kuigwa na wachezaji wenzake katika nchi hii. Atakuwa mchezaji mkubwa dunaini miaka kadhaa ijayo. Luis Suarez alikuwa katika kiwango hichi, kisha akacheza timu hii na kujipambanua zaidi na kwenda kuwa mchezaji mkubwa duniani na naweza kuona Coutinho anaelekea njia hiyo hiyo,"
0 comments:
Post a Comment