// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CHELSEA BINGWA ENGLAND, MAN CITY WA ZAMANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CHELSEA BINGWA ENGLAND, MAN CITY WA ZAMANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, May 03, 2015

    CHELSEA BINGWA ENGLAND, MAN CITY WA ZAMANI

    CHELSEA imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace Uwanja Stamford Bridge, London jioni ya leo.
    Chelsea imefikisha pointi 83 baada ya kucheza mechi 35. Chelsea inarithi taji la Manchester City na hakuna timu inayoweza kufikisha pointi hizo. 
    Hilo linakuwa taji la nne kwa Chelsea katika historia yao na ni furaha kubwa kwa kocha Jose Mourinho ambaye anaendelea rekodi yake nzuri. 
    Bao pekee la The Blues lilifungwa na Eden Hazard akimalizia mpira uliokolewa na kipa Julian Speroni kufuatia mkwaju wa penalti wa Mbelgiji huyo dakika ya 45. 
    Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Fabregas, Matic, Cuadrado/Mikel dk45, Willian/Zouma dk85, Hazard/Filipe Luis dk92 na Drogba. 
    Crystal Palace: Speroni, Mariappa, Dann, Delaney, Ward, Puncheon, McArthur, Ledley, Zaha, Mutch na Bolasie. 
    Eden Hazard akipiga ngumi hewani akiwa na Nemanja Matic (kulia) baada ya kuifungia Chelsea bao la ubingwa dhidi ya Crystal Palace leo

    PICHA ZAIDI NENDA: 

    http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3066184/Chelsea-1-0-Crystal-Palace-Blues-clinch-Premier-League-title-Eden-Hazard-heads-home-seeing-initial-penalty-saved.html#ixzz3Z5O3V0DZ 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA BINGWA ENGLAND, MAN CITY WA ZAMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top