![]() |
Rais wa TFF, Jamal Malinzi akiwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou |
Uenyeji huu ni hatua muhimu sana kwa Tanzania katika kukuza soka la vijana na kwa hatua hii Tanzania itacheza moja kwa moja fainali hizi.
Katika kuandaa kikosi bora cha kushiriki fainali hizi Tanzania, mwezi Juni mwaka huu TFF itaandaa mashindano ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 13 na wachezaji bora wa mashindano haya wataunda kikosi cha mwanzo cha Taifa kuelekea fainali za mwaka 2019.
TFF imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fennela Mukangara kwa mchango wao wakati wa kuomba uneyeji.
TFF pia inaamini ushirikiano huo wa Serikali na wadau wengine utafanikisha mashindano haya mwaka 2019. Hii ni mara ya kwanza kihistoria Tanzania kuwa mwenyeji wa Fainali za za Mataifa ya Afrika.
0 comments:
Post a Comment