![]() |
Wachezaji wa Botswana (jezi ya bluu) na Afrika Kusini (jezi ya njano) wakiwania mpira juu Jumapili |
Namibia imewatoa mabingwa watetezi Zambia kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0, wakati Botswana imewatoa wenyeji Afrika Kusini kwa penalti 7-6 baada ya sare ya bila mabao pia.
Afrika Kusini na Zambia sasa wanaangukia kwenye Nusu Fainali za vibonde, maarufu kama michuano ya Plate na wataungana na timu zitakazofungwa Jumatatu.
Robo Fainali za michuano hiyo zitaendelea Jumatatu kwa Ghana kumenyana na vinara wa Kundi B, Madagascar Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace Saa 11: 00 jioni.
Robo Fainali ya mwisho itafuatia kwa mchezo kati ya Msumbiji na Malawi Uwanja huo huo, Royal Bafokeng Sports Palace Saa 1:30 usiku.
![]() |
Mchezaji wa Zambia (kijani) akipiga mpira mbele ya mchezaji wa namibia (nyekundu) |
0 comments:
Post a Comment