TIMU ya Barcelona imetwaa taji la pili msimu huu, baada ya usiku huu kuifunga Athletic Bilbao mabao 3-1 katika fainali ya Kombe la Mfalme, maarufu kama Copa del Rey Uwanja wa Nou Camp.
Lionel Messi aliwapangua mabeki wanne kuifungia Barcelona bao zuri la kwanza dakika ya 20, kabla ya Mbrazil Neymar kufunga la pili dakika ya 36.
Nyota wa Argentina, Messi akakamilisha ushindi mnono wa Barca ambao tayari wana taji la La Liga kwa bao zuri dakika ya 74, wakati bao la kufutia machozi la Bilbao lilifungwa na Williams dakika ya 79.
Barca sasa inarudi kwenye maandalizi ya kujaribu kutwaa taji la tatu, itakapokutana na Juventus katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa; Ter Stegen; Alves, Pique, Mascherano, Jordi Alba/Mathieu, Rakitic, Busquets, Iniesta/Xavi, Messi, Suarez/Pedro na Neymar.
Athletic Bilbao; Herrerin, Bustinza, Etxeita, Laporte, Balenziaga, San Jose, Benat/Ibai, Iraola, Rico/Iturraspe, Williams na Aduriz.
0 comments:
Post a Comment