Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
KIUNGO Said Hamisi Ndemla, amesema kwamba ataongeza juhudi ili kukuza kiwango chake na aweze kuisaidia timu yake, Simba SC kushinda mataji msimu ujao.
Akizungumza baada ya kusaini Mkataba mpya wa miaka mitatu na Wekundu wa Msimbazi leo, Ndemla amesema kwamba hiyo ni changamoto mpya kwake.
“Kazi yangu nzuri katika msimu huu imeishawishi klabu kunipa Mkataba mpya. Hii ni changamoto kwangu, sasa naamini natakiwa kuongeza bidii ya mazoezi ili kukuza kiwango changu na kuisaidia timu yangu,”amesema.
Ameongeza; “Tuna kiu ya mataji, haswa taji la Ligi Kuu (ya Vodacom Tanzania Bara). Dhamira yetu kubwa msimu ujao tufanikishe azma hiyo. Tunataka ubingwa wa Ligi Kuu,”amesema.
Aidha, Ndemla zao la mradi wa soka ya vijana ya SImba SC, amewashukuru viongozi, wachezaji wenzake na benchi la Ufundi kwa ushirikiano wao kwake, ambao umemfanya leo awe mchezaji maarufu.
“Nawashukuru makocha wangu, haswa Matola (Suleiman) ambaye tulikuwa naye tangu Simba B. lakini nawashukuru viongozi kwa kuniamini, na mimi nawaahidi baada ya kusaini, nitaongeza bidii niisaidie timu,”amesema.

Said Ndemla akisaini Mkataba mbele ya Rais wa klabu, Evans Aveva leo |
Ameongeza; “Tuna kiu ya mataji, haswa taji la Ligi Kuu (ya Vodacom Tanzania Bara). Dhamira yetu kubwa msimu ujao tufanikishe azma hiyo. Tunataka ubingwa wa Ligi Kuu,”amesema.
Aidha, Ndemla zao la mradi wa soka ya vijana ya SImba SC, amewashukuru viongozi, wachezaji wenzake na benchi la Ufundi kwa ushirikiano wao kwake, ambao umemfanya leo awe mchezaji maarufu.
“Nawashukuru makocha wangu, haswa Matola (Suleiman) ambaye tulikuwa naye tangu Simba B. lakini nawashukuru viongozi kwa kuniamini, na mimi nawaahidi baada ya kusaini, nitaongeza bidii niisaidie timu,”amesema.
0 comments:
Post a Comment