// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC YAILIPUA YANGA SC 2-1 NA KUKATA TIKETI YA CAF, SIMBA SC WATASUBIRI SANAA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC YAILIPUA YANGA SC 2-1 NA KUKATA TIKETI YA CAF, SIMBA SC WATASUBIRI SANAA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, May 06, 2015

    AZAM FC YAILIPUA YANGA SC 2-1 NA KUKATA TIKETI YA CAF, SIMBA SC WATASUBIRI SANAA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    AZAM FC imekata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa Yanga SC jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Ushindi huo, unaifanya Azam FC ifikishe pointi 48 baada ya kucheza mechi 25, nyuma ya mabingwa, Yanga SC wenye pointi 55 za mechi 25.
    Simba SC ipo nafasi ya tatu kwa pointi zake 44 na hata ikishinda mechi yake ya mwisho itafikisha 47, hivyo kwa mwaka wa tatu mfululizo Wekundu wa Msimbazi watakosa michuano ya Afrika.
    Winga wa Azam FC, Brian Majwega akimtoka beki wa Yanga SC, Juma Abdul jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

    Mrisho Ngassa wa Yanga SC akijaribu bila mafanikio kufunga langoni mwa Azam FC



    Beki wa Azam FC akimdhibiti winga wa Yanga SC, Andrey Coutinho

    Azam FC ilitoka nyuma kwa 1-0 baada ya Mbrazil Andrey Coutinho kutangulia kuifungia Yanga SC dakika ya 12 na Bryson Raphael akasawazisha dakika ya 14 kabla ya Aggrey Morris kufunga la ushindi dakika ya 85.
    Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Gadiel Michael, Shomary Kapombe, Aggrey Morris, Mudathir Yahya, Brison Raphael, Frank Domayo, Gaudence Mwaikimba, Kipre Tchetche na Brian Majwega.  
    Yanga SC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Pato Ngonyani, Saum Telela, Danny Mrwanda, Nizar Khalfan, Amissi Tambwe, Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAILIPUA YANGA SC 2-1 NA KUKATA TIKETI YA CAF, SIMBA SC WATASUBIRI SANAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top