Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
MWANAMUZIKI mkongwe nchini, Tshimanga Kalala Assosa (pichani juu) Jumapili anatarajiwa kufanya uzinduzi wa kitabu kilichokuwa kikisubiriwa na watu wengi sana kwa muda mrefu mno.
Uzinduzi wa kitabu hicho cha ‘Jifunze LINGALA kwa Kiswahili’, utaambatana na tukio kubwa la wana Dar Kavasha Club pamoja na chakula cha jioni cha pamoja ndani ya ukumbi wa MRC Jumapili kuanzia saa 12:00 jioni hadi Saa 3:00 usiku.
MRC ndio ukumbi ambao "Club Raha Leo Show" ya TBC1 ilikuwa inafanyikia.
Assosa amewahi kupigia bendi nyingi kubwa hapa Afrika kama Negros-Success (akiwa na Bolhen na Bavon Marie), Orchestre Lipua Lipua, Orchestre Les Kamale (akiwa na Nyboma, Mulembu na Kizunga) pamoja na Fukafuka zote za Jamhuri ya KIdemokrasia ya Kongo (DRC).
Kwa Tanzania amefanya kazi na Mlimani Park Orchestra, Marquis Original, Orchestre Makassy, Orchestre Mambo Bado, Legho Stars na Bana Maquis.

0 comments:
Post a Comment