TIMU ya Arsenal imelazimishwa sare ya bila kufungan na Sunderland Uwanja wa Emirates usiku huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Matokeo hayo yanayoiongezea ponti moja Black Cats na kufikisha 38 baada ya mechi 37, yanainusuru timu hiyo kuteremka daraja msimu huu.
Kwa upande wake, Arsenal wanaofikisha pointi 72 baada ya mechi 37 pia, wanaweza kumaliza katika nafasi ya tatu, iwapo Manchester United itashindwa kuifunga Hull City Jumapili.
Kikosi cha Dick Advocaat kina kila sababu ya kumshukuru kipa wake, Costel Pantilimon kwa kuokoa michomo mingi ya hatari hadi kupata sare hiyo ya ugenini.
Pazia la Ligi Kuu England litafungwa Jumapili kwa mechi kati ya Stoke City na Liverpool Uwanja wa Britannia, Newcastle United na West Ham United Uwanja wa St. James' Park, Manchester City na Southampton Uwanja wa Etihad, Leicester City na Queens Park Rangers Uwanja wa King Power, Hull City na Manchester United Uwanja wa The KC, Everton na Tottenham Hotspur Uwanja wa Goodison Park, Crystal Palace na Swansea City Uwanja wa Selhurst Park, Chelsea na Sunderland Uwanja wa Stamford Bridge, Aston Villa na Burnley Uwanja wa Villa Park na Arsenal na West Bromwich Albion Uwanja wa Emirates, mecho zote zikianza Saa 10:00 jioni.
Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud akipiga shuti mbele ya Nahodha wa Sunderland, John O'Shea leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment