KLABU ya Arsenal imefanikiwa kutetea Kombe la FA baada ya kuichapa mabao 4-0 Aston Villa katika mchezo wa Fainali usiku huu Uwanja wa Wembley, London.
Mshambuliaji Theo Walcott aliifungia bao la kwanza Arsenal dakika tano kabla ya mapumziko na Alexis Sanchez akafunga la pili dakika tano baada ya kipindi cha pili.
Beki Mjerumani, Per Mertesacker naye akaifungia bao la tatu timu ya Arsene Wenger dakika ya 61, kabla ya Olivier Giroud aliyetokea benchi kufunga la nne dakika ya 90.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Cazorla, Ramsey, Ozil/Wilshere dk76, Sanchez na Walcott/Giroud dk76.
Aston Villa: Given, Hutton, Okore, Vlaar, Richardson/Bacuna dk67, Cleverley, Westwood/Sanchez dk70, Delph, N'Zogbia/Agbonlahor dk52, Benteke na Grealish.
Alexis Sanchez akiruka juu kushangilia baada ya kuifungia The Gunners katika ushindi wa 4-0 Kombe la FA PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment