Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imemteua Mwenyekiti wa zamani wa chama hicho, Boniface Wambura Mgoyo kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Mabadiliko ya Katiba yake
Taarifa ya Katibu Mkuu TASWA, Amir Mhando imesema kwamba uteuzi huo ulifanyika katika Mkutano wa Kamati ya Utendaji uliofanyika hivi karibuni na kujadili mambo mbalimbali ya ustawi wa chama.
Wambura alikuwa Mwenyekiti wa TASWA kuanzia Februari mwaka 2004 hadi Agosti 2010, pia amepata kukaimu nafasi ya Uenyekiti wa TASWA kuanzia mwaka 2003 hadi Uchaguzi Mkuu ulipofanyika mwaka 2004. Kwa sasa Wambura ni Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Mhando amesema TASWA inatambua Wambura licha ya kuwa na taaluma ya uandishi wa habari, ni mwanasheria, hivyo inaamini uzoefu wake ndani ya TASWA pamoja na TFF ambako amewahi kuwa Katibu wa Kamati ya Mabadiliko ya Katiba ya shirikisho hilo utasaidia sana kupata katiba nzuri.
Wajumbe wengine wa kamati hiyo yenye jumla ya watu watano ni Mhadhiri Msaidizi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano Kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Egbert Mkoko.
Mkoko kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA. Wengine ni Mhariri wa habari za michezo wa gazeti la Daily News, Nasongelya Kilyinga na Mtendaji Mkuu wa Bin Zubeiry Blogspot, Mahmoud Zubeiry, ambaye amepata kuwa Mhariri wa habari za michezo wa magazeti mbalimbali nchini.
Mwingine ni mtangazaji wa zamani wa Redio Tumaini Dar es Salaam, ambaye kwa sasa ni mfanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kitengo cha huduma kwa wateja, Domina Rwemanyila. Wajumbe wote ni wanachama wa TASWA.
“Nia ya TASWA ni kamati hiyo ifanye kazi ndani ya siku 90 ili Rasimu ya Katiba ijadiliwe katika Mkutano Mkuu wa TASWA unaotarajiwa kufanyika Julai 25 na 26 mwaka huu mkoani Morogoro.”imesema taarifa ya TASWA.
Aidha, Mhando amesema tamasha maalum kwa ajili ya wafanyakazi mbalimbali wa vyombo vya habari (Media Day Bonanza), ambalo mwaka jana halikufanyika kutokana na sababu mbalimbali, litafanyika mwaka huu likishirikisha wadau 2,000 kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Mhando amesemaa tayari kampuni mbili zimejitokeza kutaka kudhamini bonanza hilo, lakini si kwa kiwango ambacho chama kinataka na kutokana na hali hiyo, mazungumzo bado yanaendelea na wadhamini hao ambao wametoa masharti ya kupunguza idadi ya washiriki kutoka 2,000 hadi 500.
TASWA inaona idadi hiyo ni ndogo na kwa kadri watu walivyo na hamu ya kujumuika pamoja inaweza isikate kiu ya wanahabari na inaweza kuleta malalamiko kwa watakaokosa.
“Nia ya TASWA ni kuwaweka pamoja waandishi wa habari za afya, siasa, uchumi, michezo, mazingira na nyinginezo pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali kujadili masuala yanayowahusu na kisha kuburudika kwa pamoja,”.
“Kutokana na hali hiyo TASWA imekubaliana na wadhamini hao, watafutwe wadhamini wengine waongeze nguvu na kufanya bonanza hilo liwe la aina yake na tuna imani katika wiki chache zijazo suala la Media Day litakuwa limekamilika,”.
Mhando amesema kwa mazingira hayo Kamati ya Utendaji katika kurahisisha jambo hilo, imeunda kamati maalaum ambayo Mwenyekiti wa TASWA FC, Majuto Omary atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Media Day na Katibu wake atakuwa Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando.
Katika hatua nyingine, TASWA inaendelea na programu za mafunzo kwa waandishi wa habari za michezo, ambapo awamu ya kwanza ilifanyika Machi 25 mwaka huu na kuhusisha washiriki 40, ambapo 30 walikuwa chipukizi na 10 wa kada ya kati.
Awamu nyingine mbili zinatarajiwa kufanyika mwezi ujao, ambapo awamu ya kwanza itakuwa Dar es Salaam mapema mwezi ujao ikihusisha washiriki 40 kati yao 30 ni wa kada ya kati na 10 wakiwa waandishi wazoefu. Awamu ya pili itafanyika mwishoni mwa mwezi huo.
KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) imemteua Mwenyekiti wa zamani wa chama hicho, Boniface Wambura Mgoyo kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Mabadiliko ya Katiba yake
Taarifa ya Katibu Mkuu TASWA, Amir Mhando imesema kwamba uteuzi huo ulifanyika katika Mkutano wa Kamati ya Utendaji uliofanyika hivi karibuni na kujadili mambo mbalimbali ya ustawi wa chama.
Wambura alikuwa Mwenyekiti wa TASWA kuanzia Februari mwaka 2004 hadi Agosti 2010, pia amepata kukaimu nafasi ya Uenyekiti wa TASWA kuanzia mwaka 2003 hadi Uchaguzi Mkuu ulipofanyika mwaka 2004. Kwa sasa Wambura ni Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Bin Zubeiry kulia ameteuliwa Kamati ya Katiba ya TASWA |
Mhando amesema TASWA inatambua Wambura licha ya kuwa na taaluma ya uandishi wa habari, ni mwanasheria, hivyo inaamini uzoefu wake ndani ya TASWA pamoja na TFF ambako amewahi kuwa Katibu wa Kamati ya Mabadiliko ya Katiba ya shirikisho hilo utasaidia sana kupata katiba nzuri.
Wajumbe wengine wa kamati hiyo yenye jumla ya watu watano ni Mhadhiri Msaidizi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano Kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Egbert Mkoko.
Mkoko kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA. Wengine ni Mhariri wa habari za michezo wa gazeti la Daily News, Nasongelya Kilyinga na Mtendaji Mkuu wa Bin Zubeiry Blogspot, Mahmoud Zubeiry, ambaye amepata kuwa Mhariri wa habari za michezo wa magazeti mbalimbali nchini.
Mwingine ni mtangazaji wa zamani wa Redio Tumaini Dar es Salaam, ambaye kwa sasa ni mfanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kitengo cha huduma kwa wateja, Domina Rwemanyila. Wajumbe wote ni wanachama wa TASWA.
“Nia ya TASWA ni kamati hiyo ifanye kazi ndani ya siku 90 ili Rasimu ya Katiba ijadiliwe katika Mkutano Mkuu wa TASWA unaotarajiwa kufanyika Julai 25 na 26 mwaka huu mkoani Morogoro.”imesema taarifa ya TASWA.
Aidha, Mhando amesema tamasha maalum kwa ajili ya wafanyakazi mbalimbali wa vyombo vya habari (Media Day Bonanza), ambalo mwaka jana halikufanyika kutokana na sababu mbalimbali, litafanyika mwaka huu likishirikisha wadau 2,000 kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Mhando amesemaa tayari kampuni mbili zimejitokeza kutaka kudhamini bonanza hilo, lakini si kwa kiwango ambacho chama kinataka na kutokana na hali hiyo, mazungumzo bado yanaendelea na wadhamini hao ambao wametoa masharti ya kupunguza idadi ya washiriki kutoka 2,000 hadi 500.
TASWA inaona idadi hiyo ni ndogo na kwa kadri watu walivyo na hamu ya kujumuika pamoja inaweza isikate kiu ya wanahabari na inaweza kuleta malalamiko kwa watakaokosa.
“Nia ya TASWA ni kuwaweka pamoja waandishi wa habari za afya, siasa, uchumi, michezo, mazingira na nyinginezo pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali kujadili masuala yanayowahusu na kisha kuburudika kwa pamoja,”.
“Kutokana na hali hiyo TASWA imekubaliana na wadhamini hao, watafutwe wadhamini wengine waongeze nguvu na kufanya bonanza hilo liwe la aina yake na tuna imani katika wiki chache zijazo suala la Media Day litakuwa limekamilika,”.
Wambura kushoto atakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba ya TASWA |
Katika hatua nyingine, TASWA inaendelea na programu za mafunzo kwa waandishi wa habari za michezo, ambapo awamu ya kwanza ilifanyika Machi 25 mwaka huu na kuhusisha washiriki 40, ambapo 30 walikuwa chipukizi na 10 wa kada ya kati.
Awamu nyingine mbili zinatarajiwa kufanyika mwezi ujao, ambapo awamu ya kwanza itakuwa Dar es Salaam mapema mwezi ujao ikihusisha washiriki 40 kati yao 30 ni wa kada ya kati na 10 wakiwa waandishi wazoefu. Awamu ya pili itafanyika mwishoni mwa mwezi huo.
0 comments:
Post a Comment