KOCHA wa Manchester United, Louis van Gaal amesema sasa wanajiamini zaidi kuliko wapinzani wao, Manchester City katika Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa 13 nyumbani na sasa Mholanzi huyo anataka kuendeleza moto huo.
Miamba hiyo ya Jiji la Manchester itakutana Jumapili wiki hii Uwanja wa Old Trafford katika mchezo ambao, atakayeshinda atakaa juu ya mwenzake mwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Ushindi mzuri wa mabao 3-1 dhidi ya Aston Villa mwishoni mwa wiki, uliotokana na mabao mawili ya kiungo Ander Herrera na moja la mshambuliaji Wayne Rooney, umeifanya United iivuke Manchester City katika msimamo wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu Novemba 23, mwaka 2013.
Ukirejea Januari 10 mwaka huu namna timu hizo zilivyokuwa zinaachana kwa pointi 10, sasa mambo yamebadilika mno.
Louis van Gaal amesema sasa wanajiamini kuliko wapinzani wao, Manchester City ambao leo wanamenyana na Crystal Palace
Van Gaal anaamini wachezaji wa Manchester City watakuwa wamepoteza hali ya kujiamini
"Inachangia kiasi fulani katika morali ya wachezaji — kwa wapinzani wetu, lakini pia wachezaji wetu," amesema Van Gaal. Tunajiamini zaidi kwa sasa na ikiwa watapoteza pointi dhidi ya Crystal Palace, pia itabaki katika fikra zao," amesema Van Gaal.
Itawezekana kwa City kumaliza ndani ya nafasi nne za juu? Wanakutana na Crystal PalaceJumatatu jioni na Van Gaal anaamini kushuka chini kwa nafasi mbili, kisaikolojia kutakiathiri kikosi cha Manuel Pellegrini. Hata ikiwa City itashinda Uwanja wa Selhurst Park, jinsi gani watamudu shughuli ya Jumapili ijayo?
"Siwafahamu vizuri sana wachezaji mmoja mmoja wa Manchester City, siwezi kuwazungumzia. Lakini tunajiamini kiasi cha kutosha na hatujafungwa mara nyingi nyumbani. Mechi ijayo itakuwa ya kuamua,".
Van Gaal anafahamu historia ya karibuni dhidi ya wapinzani wao hao si nzuri kwa United. Wamepoteza mechi saba kati ya tisa zilizopita za mahasimu wa Jiji la Manchester, ikiwemo zote nne zilizopita.
Mara ya mwisho United kuifunga City nyumbani Uwanja wa Old Trafford ilikuwa ni Februari mwaka 2011, Rooney alipofunga bao zuri la tika tak.
Manchester United haijafunga tena City Uwanja wa Old Trafford tangu Wayne Rooney afunge bao zuri la tika tak Februari mwaka 2011


.png)
0 comments:
Post a Comment