KLABU ya Manchester United imeanza kumsaka mrithi wa muda mrefu wa Michael Carrick, huku Ilkay Gundogan akionekana kuongoza katika kuwania naafasi hiyo.
Kocha Louis van Gaal amekuwa akibutiwa mno na mchango wa Carrick Old Trafford msimu huu. Kiungo huyo wa kimataifa wa England amekuwa katika kiwango kizuri na tegemeo la klabu hiyo.
Lakini akiwa ana umri wa miaka 33, Mholanzi huyo anafahamu kiungo huyo anaelekea ukingoni, na wakati mwingi amekuwa akiandamwa na maumivu yanayomuweka nje ya Uwanja. United itamwaga noti ndefu kumsajili mrithi wa Carrick.
Lakini akiwa ana umri wa miaka 33, Mholanzi huyo anafahamu kiungo huyo anaelekea ukingoni, na wakati mwingi amekuwa akiandamwa na maumivu yanayomuweka nje ya Uwanja. United itamwaga noti ndefu kumsajili mrithi wa Carrick.
Kiungo wa Dortmund, Gundogan amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na United. Van Gaal anaihusudu ligi ya Bundesliga na anaamini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ana uwezo wa kuvaa viatu vya Carrick kwa muda mrefu.
Carrick, ambaye hivi karibuni amesaini Mkataba wa miezi 12 zaidi, ataendelea kuwa ndani ya mipango ya Van Gaal kwa msimu ujao - lakini klabu inajipanga kwa maisha bila yeye.
Kocha wa United, Louis van Gaal amekuwa akivutiwa na mchango wa Carrick katika timu
Van Gaal amemtambulisha kiungo wa Borussia Dortmund, Ilkay Gundogan kama mrithi wa muda mrefu wa Carrick
Kocha wa Borussia, Jurgen Klopp asingependa kuona kiungo huyo anaondoka katika kikosi cha Dortmund, lakini Mkataba wake wa sasa Gundogan unamalizika mwishoni mwa msimu ujao na hadi sasa hajasaini Mkataba mpya.
Dortmund iko tayai kumtia pingu mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, lakini tu itasikiliza ofa ili kuepuka kumuachia bure mwaka 2016.
0 comments:
Post a Comment