// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); URENO YAPIGWA 2-0 NA CAPE VERDE NYUMBANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE URENO YAPIGWA 2-0 NA CAPE VERDE NYUMBANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, April 01, 2015

    URENO YAPIGWA 2-0 NA CAPE VERDE NYUMBANI

    URENO imefungwa na timu ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1986 kufuatia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Cape Verde jana katika mchezo ambao ilimkosa Nahodha wake, Cristiano Ronaldo.
    Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Antonio Coimbra da Mota mjini Estoril, mabao ya Cape Verde inayoshika nafasi ya 37 katika viwango vya FIFA, yalifungwa na Odair Fortes na Gege kipindi cha kwanza.
    Beki wa Ureno, Andre Pinto alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 60 kwa kucheza rafu.
    Kikosi cha Ureno kilikuwa; Lopes, Cedric, Andre Pinto, Oliveira, Antunes, Adrien/Pizzi dk65, Andre Gomes/A Almeida dk79, Joao Mario/Ukra dk46, Bernardo Silva/Danilo dk61, Vieirinha na Almeida/Eder dk64.
    Cape Verde; Vozinha, Jeffrey, Varela/Calu dk71, Gege/Steven dk56, Nivaldo, Nuno, Semedo, Julio/Ryan Mendes dk81, Platini/Babancao dk62, Odair Fortes/Garry dk80 na Heldon/Ricardo Gomes dk81.
    Cape Verde Islands defender Gege celebrates after scoring the second goal against Portugal on Tuesday
    Beki wa Cape Verde, Gege akishangilia na wenzake baada ya kuifungia timu yake dhidi ya Ureno jana

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3020508/Portugal-0-2-Cape-Verde-Islands-African-nation-shock-Fernando-Santos-Cristaino-Ronaldo-sits-friendly.html#ixzz3W2lPbMxd 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: URENO YAPIGWA 2-0 NA CAPE VERDE NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top