// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TWIGA STARS NA ZAMBIA KURUDIANA APRILI 10 TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TWIGA STARS NA ZAMBIA KURUDIANA APRILI 10 TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, April 02, 2015

    TWIGA STARS NA ZAMBIA KURUDIANA APRILI 10 TAIFA

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) Aprili 10,  mwaka huu, itashuka dimbani  Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwakarisbisha Zambia (The She-Polopolo) katika mchezo wa marudiano kufuzu Fainali za Afrika.
    Twiga Stars inayonolewa na kocha mkuu Rogasian Kaijage iliingia kambini mwishoni mwa wiki na kikosi cha wachezaji 25 katika hostel za TFF zilizopo Karume, kujiandaa na mchezo huo ambao ni muhimu wa kuwania kufuzu kwa fainali za michezo ya Afrika mwaka huu.
    Wachezaji wa Twiga Stars wakiwa mazoezini Uwanja wa Karume, Dar ves Salaam hivi karibuni

    Katika mchezo wa awali uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Lusaka Zambia, Twiga Stars iliibuka na ushindi wa mabao 4-2, mabao yaliyofungwa na Asha Rashid (2), Shelder Boniface (1) na Sophia Mwasikili (1).
    Mshindi wa jumla katika mchezo huo atafuzu moja kwa moja kwa fainali za Michezo ya Afrika zitakazofanya nchini Congo - Brazzavile kuanzia Septemba 13 mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TWIGA STARS NA ZAMBIA KURUDIANA APRILI 10 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top