Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), leo hii limepokea maombi toka Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), likiitaka Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ngazi ya vilabu yatakayotimua vumbi kuanzia mwezi Julai mwaka huu.
Kufuatia maombi hayo ya uenyeji wa michuano ya CECAFA kwa ngazi za vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame CUP), TFF inatafakari juu ya maombi hayo na itayatolea maamuzi.
Mara ya mwisho, michuano hiyo ilifanyika Tanzania mwaka 2012 na Yanga SC wakaibuka mabingwa, Azam FC washindi wa pili.
Mwaka uliofuata yalifanyika Sudan na Vital’O ya Burundi wakawa mabingwa, wakati mwaka jana yalifanyika Rwanda na El Merreikh ya Sudan wakabeba taji.

0 comments:
Post a Comment