// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TFF, VIONGOZI UWANJA WA TAIFA UNAFIKI UTAWAPELEKA PABAYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TFF, VIONGOZI UWANJA WA TAIFA UNAFIKI UTAWAPELEKA PABAYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, April 28, 2015

    TFF, VIONGOZI UWANJA WA TAIFA UNAFIKI UTAWAPELEKA PABAYA

    Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
    YAWEZEKANA kabisa Shirikisho la Soka Nchini TFF limejiwekea `mitego` yake yakujipatia Fedha kwa Njia za `Panya`. Labda kwakuona Njia halali haziziingizii Fedha za kutosha au kutokuridhika kwao,au `Ulafi` tu au vyote kwa Pamoja.
    Na Pale Uwanja wa Taifa kuna ufisadi unaendelea ambao baadaye ni lazima itakuwa kama `Escrow`. Na Ndiyo maana kuna matajiri wakupindukia  ambao hutumia milioni 20 kusherehea siku ya kuzaliwa na wapo watanzania wanalala wakiwaza asubuhi watapata wapi elfu moja ya chai na Muhogo.
    TFF hii ya Tanzania Ndiyo Shirikisho lenye `vituko` pekee si tu Barani Afrika bali pia ulimwenguni kwa ujumla kutokana na mienendo yake kila kukicha. Sitaki kuamini na wala sijasema kama kule Ndani ya  TFF kuna `wendawazimu` au laa. (ila naamini kuna wasomi!)
    Kuna kanuni Mbalimbali zimwekwa na Shirikisho hilo ikiwa ni Nzuri au mbaya ilimradi kuonyesha mchezo wa Soka unaendeshwa kwa Sheria na Kanuni zake nani mchezo unaoheshimika.
    Beki wa Yanga SC Juma Abdul kulia katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa
    Mrisho Ngassa wa Yanga SC kushoto katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa

    Inachokifanya TFF siyo jambo geni  kwakuwa hata FIFA kuna Sheria na Kanuni ingawa Sheria kutoka FIFA yaweza  kutumika katika kila Shirikisho na Shirikisho husika hujiwekea Kanuni zake.
    Kuna zaidi ya wachezaji  10 wanaocheza timu za Ligi kuu ya soka Tanzania Bara ambao tayari `wameumwa` na adhabu mbalimbali ikiwamo kwakutozwa Fedha ama kufungiwa michezo kadhaa ama vyote kwa pamoja.
    Ni sahihi kwakuwa hakuna  chombo chaweza kuendeshwa bila kuwa na kanuni ama sheria. Nchi hii isingekuwa na kanuni  au sheria basi tungekatana `mapanga` sana. Kwa Nchi hii inavyokwenda kama kusingalikuwepo na sharia  naamini ningekuwa `gerezani` kwakuwa  Ningeanza kukata kata baadhi ya watu Ndani ya Shirikisho hilo kwa mambo yao ya`kipuuzi` wanayofanya ambayo hufubaza Soka letu Nchini.
    Baadhi ya Waamuzi nao hufuata sharia 20 badala ya 17 za Soka,huja na sharia zao mifukoni na kuonyesha maajabu Viwanjani, Viongozi au wachezaji wakilalamika bs kamati zilizowekwa na TFF huwachukua hatua za kuwatoza fedha.
    Unaweza kujiuliza mbona katika Nchi za wenzetu hatuoni wachezaji au Viongozi wa timu wakiwalalamikia waamuzi kiasi kikubwa? Jibu ni rahisi, hakuna malalamiko mengi kwakuwa waamuzi wengi nao hufuata sheria 17 za Soka.
    Baadhi ya vumba vya kubadilishia mavazi wanazoingia wachezaji  ni vibovu,vichafu,hewa ndogo lakini timu zisipoingia vyumbani hutozwa Fedha. Inaonekana ni kama mradi wa TFF.
    Lakini TFF yetu haijisumbui kwenda kuhakikisha malalamiko ya timu zinazokwepa kuingia vyumbani,wao huwaza fedha .
    Wakati wa mapumziko wachezaji hutoka jasho jingi,huitaji kupata hewa safi kwa wingi. Sasa wanapoingia tena katika vyumba vilivyobana hewa,harufu chafu ,unataka kuwapotezea maisha? Kwanini msiwachukulie hatua wahusika? Ni kama `uwendawazimu` unaofanywa na baadhi ya  viongozi wa uwanja wa Taifa, kuna makato ya usafi wa uwanja hufanywa kila mchezo,na katika makaratasi  inaonyesha kila mfanyakazi anapata elfu 30 lakini ukweli ni kwamba kila mfanyakazi anapata elfu tano tu 5000, tena siyo kila mchezo unaochezwa. Hi Nchi ukiwa tajiri utaendelea kuwa Tajiri tu kwasababu ya `upuuzi` kama huu na ukiwa masikini mnyonge utaendelea kuwa Mnyonge.
    Pale uwanja wa Taifa mara tu baada ya mchezo kati ya Simba na Ndanda kumalizika Ndani ya Vumba hakukuwa na umeme. Suilaumu sana kwakuwa kila mmoja anaijua TANESCO yetu. Lakini yale Makato Makubwa yanayokatwa hayajanunua Gereta!!! Elfu 30 mnazoandika kuwapa wafanyakazi na hamuwapi zipowapi? Ipo siku Mungu atawaadhibu kwa unafiki.
    Kwa Upande wa TFF ,Kama TFF itakuwa legelege lazima na soka letu litakuwa legelege kama linavyoonekana kuwa legelege kuanzia katika kanuni za `kuwanyoga` wachezaji na vilabu vyao.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi wa pili kushoto

    Mchezaji akibishana na mwamuzi basi baada ya wiki chache utasikia katozwa laki tano, vyoo vibovu lakini mchezaji asipoingia chooni anapigwa fimbo ya fedha.
    Waamuzi wana chama chao ambacho huwachukulia hatua waamuzi wanaosigina sharia,lakini idadi ya waamuzi wanaochukuliwa hatua ni ndogo na hailingani na idadi ya makosa wanayoyafanya.
    Mwamuzi wa Tanzania akitoa kadi Nyekundu katika  dakika ya 70 hata kama kadi yenyewe ilikuwa ni halali basi upande wa pili ambao wanafaidika na kadi hiyo wataanza kuonewa na mwamuzi huyohuyo. Inashangaza sana!!!
    TFF na binamu yao bodi ya ligi  hutoa ratiba ya ligi kabla ya msimu haujaanza, na wanatoa kauli wakiwa na macho makavu kuwa  haitotibua ratiba. lakini TFF hiyohiyo hutibua tena ratiba hiyo hiyo wakiwa na macho yale yale makavu. Hivi hawa  jamaa hawaangaliagi Ratiba za michuano ya kimataifa ya kirafiki ya Timu ya Taifa kabla ya kupanga Ratiba zao za ligi? Hawaangalii ratiba za CAF Kwa timu zinazowakilisha Nchi katika michuano ya kimataifa?
    Inajua miondombinu ni mibovu hasa nyakati za mvua,kule Shinyanga mvua zilikuwa kubwa baadhi ya michezo ilisogezwa mbele, lakini gharama zinabaki kwa timu kusubiri siku ya mchezo,TFF yenye kukata makato makubwa kila mchezo hapo haihusiki hata kwa shilingi moja.
    Inavyooneakana TFF imekaza macho yake katika Fedha tu na makosa yakubuni buni.

    (Mwandishi wa makala haya ni Mtangazaji wa Redio One na ITV na anapatikana kwa namba +255 655 250 157 na +255 752 250 157)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF, VIONGOZI UWANJA WA TAIFA UNAFIKI UTAWAPELEKA PABAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top