• HABARI MPYA

    Tuesday, April 07, 2015

    TENGA AIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI WA CAF

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MWENYEKITI wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga amerejea katika nafasi yake ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shiriksiho la Soka Afrika (CAF) baada ya uchaguzi uliokwenda sambamba na Mkutano Mkuu mjini Cairo, Misri Aprili 6 na 7 mwaka huu.
    Tenga, Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), sasa ataitumikia nafasi hiyo kwa miaka mingine minne kama Mkuu wa ukanda wa CECAFA. 
    Hawa ni damu damu; Tenga akifurahia kushoto na Rais wa TFF, Jamal Malinzi. Nahodha huyo wa zamani wa taifa Stars ametetea nafasi yake CAF

    Taarifa ya Katibu Mkuu wa CECAFA kwa BIN ZUBEIRY, Nicholas Musonye leo, imesema kwamba Mkutano Mkuu wa CAF ambao hufanyika kila mwaka, ulianza Jumatatu mjini Cairo na nchi zote 54 wanachama zikiwemo 12 za CECAFA zilihudhuria. 
    Wanachama wa CECAFA ni Burundi, Kenya, Uganda, Tanzania, Somalia, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Zanzibar, Rwanda, Sudan na Sudan Kusini.
    Tenga alichaguliwa bila kipingamizi, baada ya aliyekuwa mpinzani wake, Hassan Suleiman wa Djibouti kujitoa na kumsapoti Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TENGA AIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI WA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top