// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TAMBWE AWAGARAGAZA SIMBA SC ‘KIZIMBA CHA TFF’, WATAKIWA KUMLIPA MAMILIONI YAKE, VINGINEVYO WATAKOMA! - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TAMBWE AWAGARAGAZA SIMBA SC ‘KIZIMBA CHA TFF’, WATAKIWA KUMLIPA MAMILIONI YAKE, VINGINEVYO WATAKOMA! - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, April 27, 2015

    TAMBWE AWAGARAGAZA SIMBA SC ‘KIZIMBA CHA TFF’, WATAKIWA KUMLIPA MAMILIONI YAKE, VINGINEVYO WATAKOMA!

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI Amissi Tambwe ameshinda kesi dhidi ya klabu yake ya zamani, Simba SC juu ya mafao yake.
    Simba SC ilimtema mshambuliaji huyo wa Burundi ndani ya Mkataba, lakini ikashindwa kumlipa, naye akafungua kesi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    Kesi hiyo jana imesikilizwa mbele ya Kamati ya Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake, Richard Sinamtwa na Tambwe ameshinda.  
    Madai ya Tambwe jumla ni dola za Kimarekani 7,000 (Sh. Milioni 14 za Tanzania), kati ya hizo 1,000 zikiwa ni mshahara wa mwezi mmoja na nyingine za kuvunjia Mkataba.
    Tambwe akiwa na Wakili Frank Macha jana jioni ofisi za TFF, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam 

    Simba SC wamepewa hadi Aprili 30 kuwa wamemlipa Tambwe dola 5,000 na nyingine wamalizie Mei 10, mwaka huu- na wakishindwa kufanya hivyo watakatwa fedha zote mara moja katika mapato ya mechi zao.
    Tambwe aliongozana na Wakili wa klabu yake, Yanga SC, Frank Macha wakati Simba SC iliwakilishwa na Katibu wake, Stephen Ally.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAMBWE AWAGARAGAZA SIMBA SC ‘KIZIMBA CHA TFF’, WATAKIWA KUMLIPA MAMILIONI YAKE, VINGINEVYO WATAKOMA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top