Na Prince Akbar. DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya EAG Group Limited, imeingia Mkataba wa miaka mitano na Simba SC ambao utahusu kuitafutia dili klabu hiyo za kuingiza fedha.
Mkurugenzi wa EAG, Imani Kajula ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba mipango yote ya kuendesha dili hilo anaipata kutoka klabu ya Arsenal ya England, ambayo anafanya nayo kazi.
Kajula amesema katika mkataba huo anataka kuona Simba inakuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa kuitafutia vyanzo vingi vya mapato, ili iache kutegemea mapato ya mlangoni na ada za wanachama pekee.
"Ukiangalia kwa sasa, mwakani Simba itafikisha miaka 80, lakini kiuchumi haiendani na hadhi hiyo. Sasa katika mkataba huu, tunataka kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa klabu kuwa na vyanzo vingi vya mapato,"alisema Kajula.
Awali, akizungumza katika hafla hiyo, Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva amesema katika mkataba huo, wamepanga kutumia fursa hiyo kuendeleza mradi wao wa ujenzi wa Uwanja wao wa Bunju.
Aveva pia amesema anaamini mpango huo utawawezesha kuendeleza jingo lao la makao makuu liliopo Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam.

Rais wa Simba SC, Evans Aveva (kushoto) akisaini Mkataba na Mtendaji Mkuu wa EAG Group Limited, Imani Kajula kulia leo Dar es Salaam |
Aveva na Kajula wakibadilishana fomu za Mikataba |
"Ukiangalia kwa sasa, mwakani Simba itafikisha miaka 80, lakini kiuchumi haiendani na hadhi hiyo. Sasa katika mkataba huu, tunataka kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa klabu kuwa na vyanzo vingi vya mapato,"alisema Kajula.
Awali, akizungumza katika hafla hiyo, Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva amesema katika mkataba huo, wamepanga kutumia fursa hiyo kuendeleza mradi wao wa ujenzi wa Uwanja wao wa Bunju.
Aveva pia amesema anaamini mpango huo utawawezesha kuendeleza jingo lao la makao makuu liliopo Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment