// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC YAFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA, YAITWANGA KAGERA 2-1 KAMBARAGE, SASA BADO POINTI MOJA TU KUIKAMATA AZAM FC - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC YAFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA, YAITWANGA KAGERA 2-1 KAMBARAGE, SASA BADO POINTI MOJA TU KUIKAMATA AZAM FC - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Monday, April 06, 2015

        SIMBA SC YAFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA, YAITWANGA KAGERA 2-1 KAMBARAGE, SASA BADO POINTI MOJA TU KUIKAMATA AZAM FC

        Na Phillipo Chimi, SHINYANGA
        SIMBA SC wamefufua matumaini ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wa kuhamia, Kagera Sugar ya Bukoba Uwanja wa Kambarage, Shinyanga jioni ya leo.
        Simba SC sasa inafikisha pointi 35 baada ya kucheza mechi 21, ikizidiwa pointi moja tu na mabingwa watetezi, Azam FC wenye pointi 36, lakini wamecheza mechi 18. Yanga SC wenye pointi 40 za mechi 19, wapo kileleni.
        Katika mchezo huo ulioanza majira ya sa 9:00 Alasiri, dakika 45 za kwanza zilimalizika kukiwa hakuna bao.
        Ibrahim Hajib ameifungia Simba SC bao la ushindi leo Uwanja wa Kambarage, Shinyanga

        Kipindi cha pili, Simba SC ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’ dakika ya 52 baada ya kuuwahi mpira uliookolewa kufuatia shuti la Mganda, Dan Sserunkuma.
        Iliwachukua dakika 12 tu Kagera Sugar kusawazisha bao hilo, kupitia kwa mshambuliaji wake Rashid Mandawa aliyemalizia pasi nzuri ya Paul Ngway.
        Hilo linakuwa bao la 10 katika Ligi Kuu msimu huu kwa Mandawa, ambaye sasa amemkamata mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbangu- wote wakiwa nyuma ya winga wa Yanga SC, Simon Msuva anayeongoza kwa mabao yake 11.
        Ibrahim Hajib aliifungia Simba SC bao la pili kwa penalti dakika ya 71, kufuatia Erick Kyaruzi kuunawa mpira kwenye eneo la hatari katika harakati za kuokoa. 
        Kikosi cha Kagera Sugar; Agathon Anhtony, Salum Kanoni, Erick Murilo, Erick Kyaruzi, George Kavilla, Malegesi Mwangwa, Juma Mkopi/Paul Ngway, Babu Ally, Rashid Mandawa, Atupele Green na Benjamin Asukile/Adam Kingwande. 
        Simba SC; Peter Manyika, Nassor Masoud ‘Chollo’, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Joseph Owino, Awadh Juma, Ramadhani Singano ‘Messi’, Said Ndemla, Dan Sserunkuma/Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Emmanuel Okwi, Ibrahim Hajib/Ibrahim Twaha ‘Messi’.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: SIMBA SC YAFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA, YAITWANGA KAGERA 2-1 KAMBARAGE, SASA BADO POINTI MOJA TU KUIKAMATA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry