// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC WAFUFUA MATUMAINI YA CAF, WAIFUMUA MGAMBO 4-0, OKWI APIGA HAT-TRICK - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC WAFUFUA MATUMAINI YA CAF, WAIFUMUA MGAMBO 4-0, OKWI APIGA HAT-TRICK - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, April 22, 2015

    SIMBA SC WAFUFUA MATUMAINI YA CAF, WAIFUMUA MGAMBO 4-0, OKWI APIGA HAT-TRICK

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    MGANDA Emmanuel Okwi amepiga ‘hat-trick’ Simba SC ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Mgambo Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Wekundu wa Msimbazi sasa wanatimiza pointi 38 baada ya kucheza mechi 23, maana yake wamerudi kwenye mawindo ya nafasi ya pili dhidi ya mabingwa watetezi, Azam FC wenye pointi 42 za mechi 22. 
    Timu mbili za mbili katika Ligi Kuu hucheza michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), bingwa akicheza Ligi ya Mabingwa na mshindi wa pili Kombe la Shirikisho.
    Kipa Peter Manyika hakuwepo kabisa uwanjani leo na kwenye benchi mlinda mlango wa akiba alikuwa Richard Dennis, langoni akianza ‘mtu mzima’ Ivo Mapunda.
    Mkali kweli; Emmanuel Okwi aliyepiga magoti akishangilia moja ya mabao yake leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
    Emmanuel Okwi akiwania mpira dhidi ya beki wa Mgambo, Novaty Lufunga kushoto
    Beki wa Simba SC, Mohammed Hussein 'Tshabalala' akimtoka beki wa Mgambo, Ramadhan Malima

    Mgambo waliuanza vizuri mchezo wa leo na dakika ya kwanza tu kipa wa Simba SC, Ivo Mapinda alilazimika kupangua shuti kali la beki Abuu Daudi aliyepanda kusaidia mashambulizi na kuwa kona ambayo haikuwa na madhara.
    Mgambo tena dakika ya tatu walilitia majaribuni lango la Simba SC, lakini Salim Kipaga akashindwa kuunganisha mpira wa adhabu wa Fully Maganga, baada ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kumchezea rafu Salum Mlima nje kidogo ya boksi.
    Simba SC waliamka dakika ya tano na mshambuliaji Ibrahim Hajib akafunga bao kwa pasi ya kichwa ya Okwi, lakini mshika kibendera Mashaka Mwandembwa akadai alizidi.
    Okwi alifunga bao la kwanza dakika ya tisa kwa shuti kali baada ya kupokea pasi safi ya beki Hassan Kessy aliyewatoka mabeki wa Mgambo.
    Almanusra Okwi afunge tena dakika ya 11 baada ya kutumia makosa ya mawasiliano mabovu kati ya kipa wa Mgambo, Godson Mmasa na mabeki wake, lakini bahati mbaya au nzuri kwa JKT, shuti lake ‘likaota mbawa’.
    Hajibu akiwa amebaki na kipa Mmasa dakika ya 13 akamdakisha.
    Ramadhani Singano ‘Messi’ aliifungia Simba SC bao la pili dakika ya 16 kwa shuti la mpira wa adhabu lililotinga nyavuni moja kwa moja. Faulo hiyo ilitokana na Okwi kuangushwa nje kidogo ya boksi na Abuu.
    Mgambo walijibu mapigo dakika ya 19, lakini shuti la Malimi Busungu likatoka nje kidogo, baada ya pasi nzuri ya Fully Maganga.
    Awadh Juma alishindwa kuunganisha krosi safi ya Kessy dakika ya 25, baada ya shuti lake kuota mbawa.
    Okwi akaifungia SImba SC bao la tatu na la pili kwake katika mchezo huo dakika ya 41 akitumia  makosa ya mabeki wa Mgambo, Malima Busungu na Novaty Lufunga kutegeana kuokoa.
    Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Salim Aziz Gilla almanusra aiadhibu timu yake ya zamani dakika ya 43 kama si shuti lake kupaa juu kidogo ya lango akiwa ndani ya boksi. 
    Wakati refa anajiandaa kupuliza kipyenga cha kumaliza ngwe ya kwanza, Hajib alifanikiwa kumtoka hadi kipa Mmasa, lakini akapiga nje.
    Kipindi cha Wekundu wa Msimbazi walirudi na moto wa na kufanikiwa kupata bao la nne dakika ya 51, mfungaji Okwi tena akikamilisha hat-trick yake, baada ya kuwapiga chenga mabeki na kipa wa Mgambo, kufuatia pasi safi ya Hajib.
    Fully Maganga alipewa pasi nzuri na Busungu dakika ya 69 akiwa amebaki na kipa ndani ya boksi, lakini akapiga juu ya lango.
    Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Joseph Owino, Juuko Murusheed, Jonas Mkude/William Lucian ‘Gallas’ dk76, Ramadhani Singano ‘Messi’/Simon Sserunkuma dk60, Said Ndemla, Ibrahim Hajib, Emmanuel Okwi na Awadh Juma.
    Mgambo JKT; Godson Mmasa, Abuu Daudi/Bashiru Chanache dk31, Salum Mlima, Salum Kipaga, Novart Lufunga, Ramadhan Malima/Sabri Makame dk46, Ally Nassoro, Mohammed Samatta/Ayoub Saleh dk76, Malimi Busungu, Fully Maganga na Salum Gilla.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC WAFUFUA MATUMAINI YA CAF, WAIFUMUA MGAMBO 4-0, OKWI APIGA HAT-TRICK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top