// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SHERMAN FITI, KUWAVAA COASTAL UNION KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SHERMAN FITI, KUWAVAA COASTAL UNION KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
    Tuesday, April 07, 2015

    SHERMAN FITI, KUWAVAA COASTAL UNION KESHO

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI Mliberia, Kpah Sherman (pichani kulia) amepona maumivu ya nyonga yaliyokuwa yanamsumbua na sasa anatarajiwa kurejea uwanjani kesho timu hiyo ikimenyana na Coastal Union katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Sherman hakwenda Zimbabwe Yanga ilipokwenda kucheza mechi ya marudiano hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, FC Platinum kwa sababu ya maumivu ya nyonga.
    Lakini jana mshambuliaji huyo mwenye misuli ya nguvu na umbo la kimichezo haswa, aliungana na wenzake mazoezini Uwanja wa Karume baada ya kurejea kutoka Zimbabwe walipofungwa 1-0.
    Yanga imefuzu hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrka kwa jumla ya mabao 5-2, baada ya awali kushinda 5-1 Dar es Salaam.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Sherman alisema kwamba anamshukuru Mungu amepona na anatarajia Jumatano atacheza.
    “Sasa najisikia vizuri na ninaweza kucheza Jumatano leo (jana) nimefanya mazoezi na wenzangu,”amesema.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SHERMAN FITI, KUWAVAA COASTAL UNION KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry