// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); REFA ‘MBAYA’ WA TANZANIA KUCHEZESHA ETOILE NA YANGA SOUSSE, NI YULE ALIYEIUMA STARS IKAPIGWA NA MAMBAS ZIMPETO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE REFA ‘MBAYA’ WA TANZANIA KUCHEZESHA ETOILE NA YANGA SOUSSE, NI YULE ALIYEIUMA STARS IKAPIGWA NA MAMBAS ZIMPETO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, April 21, 2015

    REFA ‘MBAYA’ WA TANZANIA KUCHEZESHA ETOILE NA YANGA SOUSSE, NI YULE ALIYEIUMA STARS IKAPIGWA NA MAMBAS ZIMPETO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    REFA Mganda, Dennis Batte aliyefupisha safari ya Tanzania katika mbio za Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2015 Equatorial Guinea, ndiye atachezesha mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho baina ya wenyeji, Etoile du Sahel na Yanga SC Mei 1, mwaka huu Uwanja wa Oimpiki mjini Sousse, Tunisia.
    Batte atasaidiwa na Waganda wenzake, Mark Ssonko na Balikoowa Musa Ngobi, ambao watakuwa washika vibendera. Mwamuzi wa akiba pia atatoka huko, wakati Kamisaa atatoka nchi nyingine. 
    Batte ‘aliiuma’ Taifa Stars wazi wazi ikifungwa mabao 2-1 na wenyeji Msumbiji Agosti 3, mwaka jana Uwanja wa Zimpeto mjini Maputo katika mchezo wa marudiano, hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza fainali hizo ambazo awali ilikuwa zipigwe Morocco.

    Mbaya wetu; Refa Dennis Batte akisindikizwa na Polisi na mbwa Agosti 3, mwaka jana baada ya 'kuinyonga' Taifa Stars Uwanja wa Zimpeto.

    Taifa Stars ilitolewa katika kwa jumla ya mabao 4-3, baada ya awali kulazimishwa sare ya 2-2 Dar es Salaam na hata hivyo, Mambas hawakufurukuta katika kundi lililokuwa na Cape Verde, Niger na Zambia kuwania tiketi ya AFCON ya Januari mwaka huu.
    Batte alikataa bao zuri la kichwa la beki Said Mourad aliyeunganisha mpira wa adhabu wa Khamis Mcha ‘Vialli’ baada ya Thomas Ulimwengu kuangushwa dakika ya 17.
    Mshika kibendera nambari moja alimnyooshea kibendera cha kuotea mshambuliaji John Bocco akiwa anakwenda kufunga, wakati alikuwa hajaotea dakika ya 44.
    Bado Batte na wasaidizi wake walitumia ujanja wa kitaaluma kupunguza kasi na mipango ya Stars kusaka mabao- kwa mfano kila wachezaji walipopamiana, mpira ulielekezwa kwa Tanzania- wachezaji wa Msumbiji walikuwa wana maisha mazuri mno mbele ya marefa wa Uganda siku hiyo.
    Baada ya Mganda huyo kupuliza kipyenga cha kumaliza mchezo, wachezaji wa Stars walimfuata kumlalamikia huku wakilia kwa kile walichofanyiwa uwanjani. Wachezaji wa Stars walishindwa kuificha huzuni yao baada ya kuanza kulia uwanjani. 
    Shomary Kapombe akiwa taaban kwa kilio sababu ya Batte Agosti 3, mwaka jana Uwanja wa Zimpeto
    Shabiki akimbembeleza Mbwana Samatta Agosti 3, mwaka jana Uwanja wa Zimpeto

    Wachezaji kadhaa wa Yanga SC, Deo Munishi ‘Dida’, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Oscar Joshua, Edward Charles, Simon Msuva, Mrisho Ngassa walikuwepo kikosini Stars siku hiyo na wana kumbukumbu yote ya Batte Uwanja wa Zimpeto.
    Kama ilivyokuwa kwa Stars, Yanga SC nao wana shinikizo la kupata ushindi wa ugenini baada ya kulazimishwa sare nyumbani ya bao 1-1 mwishoni mwa wiki.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: REFA ‘MBAYA’ WA TANZANIA KUCHEZESHA ETOILE NA YANGA SOUSSE, NI YULE ALIYEIUMA STARS IKAPIGWA NA MAMBAS ZIMPETO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top