Na Phili Chimi, SHINYANGA
BAADA ya kufungwa na Bugando Dayness ya Mwanza, timu ya mpira wa kikapu ya Risasi ya hapa, imeanza kujifua kwa ajili ya mchezo wa marudiano ili walipe kisasi.
Risasi ilifungwa kwa vikapu 68-58 na wenyeji wao Bugando Dayness mjini Mwanza kwenye mchezo wa kirafiki Jumapili iliyopita na sasa timu hiyo imeanza mazoezi rasmi ili kulipa kisasi.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini hapa, Kocha Mkuu wa Risasi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Shinyanga, Henry Kisinja amesema timu hiyo kwa sasa imeanza mazoezi ya nguvu ili kujifua vyema kwa ajili ya kuja kuwakabili mahasimu wao hao kutoka Mwanza kwenye mechi ya marejeano hapa mjini Shinyanga.
Amesema wanafanya mazoezi ya nguvu kwa sababu wanakabiliwa na michezo miwili ya kirafiki dhidi ya timu kutoka Geita, michezo ambayo yote hiyo itapigwa baada ya sikukuu ya Pasaka.
Risasi kwa sasa kwa ujumla inajiandaa na michezo ya Kanda ya Ziwa inayotarajiwa kuanza Aprili mwaka huu. Timu nyingine za Shinyanga zitakazoshiriki michuano hiyo ni Kambarage ya Shinyanga Mjini, Kahama ya Kahama, Kishapu na Mwadui za Kishapu.

0 comments:
Post a Comment