// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NGASSA SASA ‘DEIWAKA’ YANGA SC, MKATABA WAKE UMEISHA RASMI JANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NGASSA SASA ‘DEIWAKA’ YANGA SC, MKATABA WAKE UMEISHA RASMI JANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, April 21, 2015

    NGASSA SASA ‘DEIWAKA’ YANGA SC, MKATABA WAKE UMEISHA RASMI JANA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KUANZIA jana, Mrisho Khalfan Ngassa (pichani kushoto) si mchezaji wa Yanga SC, kufuatia kumalizika kwa Mkataba wake.
    Lakini kwa mujibu wa kanuni za soka, ataendelea kuichezea timu hiyo kumalizia msimu, kwa kuwa amesajiliwa kucheza mashindano yote ya nyumbani na ya Afrika.
    BIN ZUBEIRY inafahamu jana, Aprili 20, Ngassa amemaliza Mkataba wake wa miaka miwili Yanga SC na hajasaini Mkataba mpya.
    “Kwa sasa sitaki kuzungumzia masuala ya Mkataba, nataka nimalize msimu kabisa ndiyo nianze mijadala ya Mkataba mpya. Mimi ni mchezaji niliyesajiliwa Yanga msimu huu. Nitamalizia msimu, baada ya hapo mengine yatafuata,”alisema Ngassa akizungumza na BIN ZUBEIRY jana.
    Kuhusu uvumi kwamba amesaini timu ya Free State Stars ya Afrika Kusini, Ngassa alisema; “Nipo kwenye mazungumzo na timu tatu, ikiwemo hiyo Free State, nyingine ya Qatar na pia nimeletewa ujumbe kwamba AS Vita (ya DRC) na Etoile nao wananifuatilia. Ndiyo maana nasema acha nimalize msimu kwanza, sina papara,”amesema.
    Lakini jana Ngassa alionekana katika ofisi za makao makuu wa klabu hiyo, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam akizungumza na Katibu, Dk. Jonas Tiboroha na alipoulizwa, naye alihoji; “Mimi ni ajabu kuonekana ofisi za mwajiri wangu?”.
    Ngassa amesistiza atakuwa tayari kuzungumzia masuala ya Mkataba mpya baada ya kumaliza kabisa msimu.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGASSA SASA ‘DEIWAKA’ YANGA SC, MKATABA WAKE UMEISHA RASMI JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top