// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NGASSA, MBUYU TWITE, NIYONZIMA WAKACHA MAZOEZI YA PASAKA YANGA, VISINGIZIO KIBAO! - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NGASSA, MBUYU TWITE, NIYONZIMA WAKACHA MAZOEZI YA PASAKA YANGA, VISINGIZIO KIBAO! - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Tuesday, April 07, 2015

        NGASSA, MBUYU TWITE, NIYONZIMA WAKACHA MAZOEZI YA PASAKA YANGA, VISINGIZIO KIBAO!

        Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
        WACHEZAJI watano wa Yanga SC hawakutokea mazoezini jana kila mmoja akipitishia sababu zake kwa Meneja Hafidh Saleh.
        Kipa Deo Munishi ‘Dida’, beki Mbuyu Twite, viungo Haruna Niyonzima, Mrisho Ngassa na mshambuliaji Danny Mrwanda wote hawakuwepo Uwanja wa Karume jioni ya jana.
        Na kila mmoja alitafuta njia ya kujisafisha kwa kumpigia simu Meneja, Hafidh Saleh kumuelezea udhuru wake.
        Hata hivyo, salamu hizo zilipofika kwa Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm alizichukulia kama ni janja ya wachezaji hao kupumzika sikukuu ya Pasaka.
        Kocha Msaidizi wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa akiongoza mazoezi jana Uwanja wa Karume. Wachezaji watano wakiwemo Mrisho Ngassa na Haruna Niyonzima hawakutokea

        Wakati kesho Yanga SC inatarajiwa kumenyana na Coastal Union Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wachezaji wote hao wanatarajiwa kutokea mazoezini leo.
        Yanga SC inahitaji ushindi kesho ili kujiimarisha katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu, hadi sasa ikiwa inaongoza kwa pointi zake 40 za mechi 19, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Azam FC wenye pointi 36 za mechi 18 na Simba SC pointi 35 za mechi 21.
        Mrisho Ngassa ni mchezaji tegemeo Yanga SC na makocha wa timu hiyo wamekuwa wakimpa maelekezo maalum

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: NGASSA, MBUYU TWITE, NIYONZIMA WAKACHA MAZOEZI YA PASAKA YANGA, VISINGIZIO KIBAO! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry