BONDIA Manny Pacquiao alikimbia nyumbani kwao baada ya baba yake kula mwa wa familia.
Nyota huyo wa Ufilipino alikuwa ana maisha magumu wakati wa utoto, na ni umasikini uliomsukumia kwenye mchezo wa ngumi za kulipwa mapema tu akiwa na umri wa miaka 14.
Na wiki hii, kocha wake, Freddie Roach amesema kwamba ameelezea misukosuko ya maisha ya bondia huyo kuelekea pambano lake na Floyd Mayweather usiku wa Jumamosi, kwa Tanzania itakuwa asubuhi ya Jumapili.
"Aliishi mtaani, ambako alikuwa ananunua maandazi (aina ya donati) katika maduka ya jumla na kuuza reja reja ili kupata fedha kujikimu,'amesema akizungumza na Yahoo.
"Alikuwa analala kwenye maboksi. Amepitia yote haya, alianza ngumi za kulipwa akiwa ana miaka 14, na muangalie jamaa alivyo leo.
"Ufilipno ni sehemu masikini, hakuna maisha bora, hakuna mfumo wa afya na kama huna kazi au fedha, kisha unafanya chochote ili kuishi.
"Manny alikimbia nyumbani baada ya baba yake kula mbwa wake,".'
Mapema wiki hii picha za Pacquiao akiwa mdogo nyumbani kwao zilivuja.
Alikimbia nyumbani kwao kuhamia Manila akacheze ngumi za kulipwa. akiwa ana umri wa miaka 36 sasa, sasa ni miongoni mwa nyota wakubwa duniani.
Zipo picha ambazo zinamuonyesha Pacquiao akifanya mazoezi katika gym ya LM mjini Manila mwaka 1996 akiwa ana umri wa miaka 17 baada ya kushinda mapambano yake 10 ya awali ya ngumi za kulipwa ambayo yote alipigana mwaka 1995.
Mwaka huo huo ambao alipigwa picha hizo, Mayweather alikuwa anajiandaa kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki mwaka 1996 mjini Atlanta, ambayo alimaliza kuwa kushindwa kwa utata na dhidi ya Serafim Todorov katika Nusu Fainali.
0 comments:
Post a Comment