MPIRA ni ni mchezo wa masikini? Ndiyo, mtu kutoka familia iliyoridhika ngumu sana kuhangaika na mpira au mchezo mwingine wowote.
Wengi kati ya wanasoka nyota duniani, ukichimba historia zao wanatoka familia duni. Narudia, mtoto kutoka familia bora vigumu kuhangaika na michezo. Wapo wachache, lakini soka haswa ni mchezo wa masikini.
Hivi sasa, huwezi kuambiwa utaje wanasoka nyota japo watatu tu halafu usilitaje jina la Neymar da Silva Santos Junior, mshambuliaji wa Barcelona na Brazil.
Namzungumzia mtu ambaye jana kafunga mabao yote mawili, Barca ikiilaza 2-0 na PSG na kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mtu ambaye, alipokuwepo kikosini Brazil ilifanya vizuri katika Kombe la Dunia, na alipokosekana ilivurunda vibaya mwaka huu katika fainali zilizofanyika nyumbani kwao.
Huyu ni tajiri sasa kwa sababu ya soka, lakini bado haipotezi ukweli kwamba ni mtoto kutoka familia duni kule Brazil.
Ni mtoto wa mwanasoka wa zamani Brazil, ambaye hakuwa na mafanikio sana, lakini akaamua kuwekeza kwa mwanaye huyo.
Na kutokana na mafanikio ya mapema ya Neymar akiwa anacheza soka ya vijana tu, aliweza kuanza kuingiza kipato mapema na kuisaidia familia yake, hatimaye kuweza kununua nyumba ya kwanza kabisa eneo la Vila Belmiro.
Mwonekano na hadhi ya familia yake viliendelea kubadilika kwa kipato cha kijana huyo na akiwa umri wa miaka 15, Neymar alikuwa anaingiza Reais 10, 000 za Brazil kwa mwezi.
Alipofikisha umri wa miaka 16, pato lake la mwezi lilipanda hadi Reais 125,000 kwa mwezi na alipofikisha umri wa miaka 17, akasaini Mkataba kamili wa mchezaji wa kulipwa katika klabu ya Santos ya kwao, Brazil.
Neymar kwa sasa ni mchezaji tajiri, ambaye familia inajivunia akiwa ana mikataba mingi ya udhamini na makampuni mbalimbali yaliyoanza kuvutiwa naye tangu ana umri wa miaka 17 kama Nike, Panasonic, Volkswagen, Tenys Pe Baruel, Lupo, Ambev, Claro, Unilever na Santander.
Wakati anaelekea kusaini Mkataba wa kujiunga na Barcelona, tayari Neymar alikuwa anashika namba 13 katika orodha ya wachezaji matajiri duniani mwaka 2012, pato lake la jumla likiwa dola za Kimarekani Milioni 18. 8 kwa miezi 12 iliyotangulia.
Mikataba yote ya udhamini aliyonayo, inamuingizia Neymar kiasi cha Euro Milioni 20 kwa mwaka na haikuwa ajabu Mei 8 mwaka 2013, SportsPro ilipomtaja Neymar kama mchezaji anayeuzika zaidi duniani, akiwapiku Lionel Messi (wa pili) na Cristiano Ronaldo (wa nane).
Lakini huyu ni mtoto kutoka familia ya kimasikini, sawa na Peter Manyika Jr., kipa bwana mdogo wa Simba SC ambaye naye amefuata nyayo za baba yake, Manyika Peter Sr.
Akiwa ana umri wa miaka 18 sasa katikaa msimu wake wa kwanza Simba SC ya Ligi Kuu ya Tanzania, Manyia Jr. habari zinazompamba zaidi ni za kimapenzi.
Ni jana tu, Manyika Jr. ametoka kuomba radhi wanachama na wapenzi wa Simba kwa maneno ya kifedhuli aliyoposti kwenye akaunti yake ya Instagram sababu ya ‘ulevi wa penzi’.
Mwishoni mwa wiki, Manyika aliposti katika akaunti yake ya Instagram kwamba yuko tayari kuondoka Simba SC, iwapo ataendelea kusakamwa kwa mahusiano yake na mpenzi wake, Naima Salum ‘Nimaa’.
Baadhi ya wadau wa Simba SC wamekuwa wakisema kipa huyo, aliyerithi glavu na umahiri wa baba yake, Manyika Peter uwezo wake umeanza kupungua tangu azame kwenye dimbwi la mapenzi ya Naima, nyota wa video za muziki nchini.
Awali, Manyika mwenyewe aliwahi kukana kuwa katika mahusiano na ‘toto hilo la kimanga’ akidai ni rafiki yake wa kawaida. Lakini baada ya kutunguliwa mara mbili Simba SC ikilala 2-0 mbele ya Mbeya City Jumamosi Uwanja wa Sokoine Mbeya, akageuza kauli.
Manyika aliposti picha katika pozi la kimahaba na Naima kwenye akaunti yake ya Instagram akiambatanisha na ujumbe; “Anayesema mrembo huyu ananiua kiwango aje kudaka yeye, kwa sababu mimi siyo hanithi, nina haki ya kuwa na mpenzi kama watu wengine, mkihisi sifanyi kazi yenu vizuri, mniache,”.
Kufatia kuenea kwa ujumbe huo, inadaiwa mlinda mlango huyo chipukizi aliitwa na viongozi wa Simba SC juzi na matokeo ya kikao chake na mabosi wake yamekuwa kuomba radhi.
“Wanadamu wengi wanafanya makosa bila kutambua kwa kuwa na upeo mdogo wa kufikiri. Wanachama na viongozi nawaomba radhi kwa kitendo nilichokifanya kijana wenu. Mnisamehe sana, naahidi kutojitokeza tena jambo hili. Nawapenda sana na ninaipenda sana Simba Sports Club. Asanteni,”.
Lakini mapema kabla ya hapo, mpenzi wake naye, Naima aliposti picha ya pozi la kimahaba na kipa huyu ikiwa imeambatana na ujumbe; “Nakupenda sana mume wangu,”.
Manyika alisajiliwa Simba SC msimu huu kama kipa wa tatu, lakini baada ya kutokea dharula ya makipa wa kwanza, Ivo Mapunda na Hussein Sharrif ‘Casillas’ kuwa majeruhi, akajikuta anaanza kazi mapema Msimbazi.
Tayari Manyika amekwishaidakia Simba SC mechi 22 za mashindano yote na kufungwa mabao 16, wakati kipa wa pili, Casillas aliyesajiliwa pia msimu huu, amedaka mechi nane tu na kufungwa mabao manne.
Kipa wa kwanza, Ivo Mapunda aliyesajiliwa Desemba mwaka juzi, hadi sasa amedaka mechi 36 na kufungwa mabao 24.
Unaweza kuona Manyika alipata fursa nzuri ya kujijengea uaminifu zaidi katika klabu yake na baada ya muda mfupi, adai Mkataba mpya ulioboreshwa kutoka ule aliosaini awali kama kipa wa tatu, tena wa timu ya vijana.
Lakini siwezi kumlaumu sana Manyika, sisi watu kutoka familia masikini furaha yetu kubwa ni mapenzi. Hata vijana ambao si wanamichezo, wanakulia katika maisha ya shida, baada ya kumaliza masomo na kupata kazi na kipato kidogo, wengi wao mambo ya awali ni mapenzi na anasa.
Neymar hakuwa hivyo. Alikuwa msaada mkubwa katika familia na alikuwa mwenye kiu, ambayo hadi sasa hajaikata. Anataka kuwa Mwanasoka Bora wa Dunia. Anataka kushinda mataji na klabu na Brazil. Anataka astaafu kama mchezaji tajiri na mwenye hadhi kubwa duniani. Lakini Tanzania kijana wa miaka 18 anahangaika na mapenzi kiasi cha kuwa limbukeni wa kuzungumza maneno ya kifedhuli. Unadhani huyo atafika wapi?

0 comments:
Post a Comment