Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
MCHEZAJI bora wa Mwaka wa Simba SC, atazawadiwa gari la sasa mwishoni mwa msimu, imeelezwa.
Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva amesema kwamba kuanzia mwisho wa msimu huu wataanzisha utaratibu wa kuwapa tuzo wachezaji wao.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo mjini Dar es Salaam, Aveva amesema kwamba mpango huo unakuja kufuatia kuingia Mkataba na Kampuni ya EAG Group Limited leo.
Simba SC leo imesaini Mkataba wa miaka mitano na EAG na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Imani Kajula ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba mipango yote ya kuendesha dili hilo anaipata kutoka klabu ya Arsenal ya England, ambayo anafanya nayo kazi.
Kajula amesema katika mkataba huo anataka kuona Simba inakuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa kuitafutia vyanzo vingi vya mapato, ili iache kutegemea mapato ya mlangoni na ada za wanachama pekee.
Aveva amesema kwamba watatoa tuzo kwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa klabu Mchezaji bora Chipukizi, sambamba na wachezaji bora wa idara tofauti kama kipa, beki, kiungo na mshambuliaji pamoja na mchezaji mwenye Nidhamu, ambao wote watapatiwa zawadi tofauti ikiwemo fedha.
"Katika tuzo hizo mchezaji bora atajinyakulia gari la kisasa, mchezaji bora kijana atapata Sh Milioni 5 huku mchezaji mwenye nidhamu akipata Sh Milioni 2 na pia tutatoa zawadi kwa mchezaji aliyetukuka, lakini washindi wote hao kila mmoja atapata na simu ya kisasa aina ya Huawei,”amesema Aveva.

Rais wa Simba SC, Evans Aveva amesema Mchezaji Bora wa Mwaka wa klabu atazawadiwa gari la kisasa |
Kajula amesema katika mkataba huo anataka kuona Simba inakuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa kuitafutia vyanzo vingi vya mapato, ili iache kutegemea mapato ya mlangoni na ada za wanachama pekee.
Aveva amesema kwamba watatoa tuzo kwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa klabu Mchezaji bora Chipukizi, sambamba na wachezaji bora wa idara tofauti kama kipa, beki, kiungo na mshambuliaji pamoja na mchezaji mwenye Nidhamu, ambao wote watapatiwa zawadi tofauti ikiwemo fedha.
"Katika tuzo hizo mchezaji bora atajinyakulia gari la kisasa, mchezaji bora kijana atapata Sh Milioni 5 huku mchezaji mwenye nidhamu akipata Sh Milioni 2 na pia tutatoa zawadi kwa mchezaji aliyetukuka, lakini washindi wote hao kila mmoja atapata na simu ya kisasa aina ya Huawei,”amesema Aveva.
0 comments:
Post a Comment