Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
REFA aliyecheza mecnhi kati ya Azam FC na Kagera Sugar, Stephen Makuka na pamoja na mshika kibendera wake namba mbili, Said Mnonga wameondolewa kwenye orodha za waamuzi wa Ligi Kuu na kufungiwa miezi 12 kwa kushindwa kumudu mchezo kwa uzembe.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 38(1) ya Ligi Kuu wakati Kamisaa wa mechi hiyo, Bevin Kapufi naye amefungiwa mwaka mmoja kwa kutoa taarifa isiyo sahihi.
Azam FC ilishinda 2-1 na Kagera wakalalamikia bao la pili lililofungwa Gaudence Mwaikimba, alikuwa ameotea akimalizia shuti la Mganda, Brian Majwega. Adhabu hiyo imetolewa kwa uzingativu wa Kanuni ya 39(1) ya Ligi Kuu.
Meneja wa Kagera Sugar, Mohamed Hussein anapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kutoa lugha ya matusi kwa waamuzi na kutaka kumpiga mwamuzi msaidizi namba 2, Said Mnonga kwenye mechi namba 158 dhidi ya Azam FC iliyochezwa Uwanja wa Azam Compex jijini Dar es Salaam.
Naye Kipa Andrew Ntala wa Kagera Sugar amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kuingia kwenye vyumba vya waamuzi na kuwatolea lugha ya matusi mazito ya nguoni baada ya mechi hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 37(5)(c) ya Ligi Kuu.

0 comments:
Post a Comment