// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MANYIKA AWAOMBA RADHI SIMBA SC, ASEMA TATIZO NI UPEO MDOGO WA KUFIKIRI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MANYIKA AWAOMBA RADHI SIMBA SC, ASEMA TATIZO NI UPEO MDOGO WA KUFIKIRI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, April 21, 2015

    MANYIKA AWAOMBA RADHI SIMBA SC, ASEMA TATIZO NI UPEO MDOGO WA KUFIKIRI

    Peter Manyika Jr. amewaomba msamaha Simba SC kupitia akaunti yake ya Intagram

    REKODI YA PETER MANYIKA SIMBA SC 

    Simba SC 0-0 Orlando Pirates (kirafiki aliingia dk43 hakufungwa, Afrika Kusini) 
    Simba SC 2-4 Bidvest Witss (Kirafiki, alifungwa nne Afrika Kusini) 
    Simba SC 0-2 Jomo Cossmos (Kirafiki, alifungwa mbili Afrika Kusini) 
    Simba SC 0-0 Yanga SC (Ligi Kuu, hakufungwa)
    Simba SC 1-1 Prisons (Ligi Kuu, alifungwa moja)
    Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu, aliokoa penalti, akafungwa moja)
    Simba SC 0-0 Express (Kirafiki, hakufungwa) 
    Simba SC 0-1 Mtibwa Sugar (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar alifungwa moja)
    Simba SC 1-0 Mafunzo (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar hakufungwa)
    Simba SC 1-0 JKU (Kombe la Mapinduzi, hakufungwa)
    Simba SC 4-0 Taifa Jang’ombe (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi, hakufungwa)
    Simba SC 1-0  Polisi (Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi, hakufungwa)
    Simba SC 0-0  Mtibwa Sugar (Alimpisha Ivo dakika ya 90, Simba ikashinda penalti 4-3 Fainali Kombe la Mapinduzi)
    Simba SC 2-0 Ndanda FC (Ligi Kuu Mtwara, hakufungwa)
    Simba SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu, alifungwa moja) 
    Simba SC 1-2 Mbeya City (Ligi Kuu Taifa, alifungwa mbili)
    Simba SC 2-0 Polisi Moro (Ligi Kuu, aliingia kipindi cha kwanza kumalizia baada ya Ivo kuumia, hakufungwa) 
    Simba SC 0-2 Mgambo Shooting (Ligi Kuu, alifungwa moja baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Ivo aliyetolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili)
    Simba SC 3-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu, hakufungwa)
    Simba SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu, aliungwa moja)
    Simba SC 3-0 Toto Africans (Kirafiki Mwanza, akiingia kipindi cha pili hakufungwa)
    Simba SC 0-2 Mbeya City (Ligi Kuu, alifungwa mbili)
    Na Princess Asia, DAR ES DALAAM
    KIPA chipukizi wa Simba SC, Peter Manyika Jr. ameomba radhi kwa maneno ya kifedhuli aliyoposti kwenye akaunti yake ya Instagram, akisema; “tatizo upeo mdogo wa kufikiri”.
    Mwishoni mwa wiki, Manyika aliposti katika akaunti yake ya Instagram kwamba yuko tayari kuondoka Simba SC, iwapo ataendelea kusakamwa kwa mahusiano yake na mpenzi wake, Naima Salum ‘Nimaa’.
    Baadhi ya wadau wa Simba SC wamekuwa wakisema kipa huyo, aliyerithi glavu na umahiri wa baba yake, Manyika Peter uwezo wake umeanza kupungua tangu azame kwenye dimbwi la mapenzi ya Naima, nyota wa video za muziki nchini.
    Awali, Manyika mwenyewe aliwahi kukana kuwa katika mahusiano na ‘toto hilo la kimanga’ akidai ni rafiki yake wa kawaida. Lakini baada ya kutunguliwa mara mbili Simba SC ikilala 2-0 mbele ya Mbeya City Jumamosi Uwanja wa Sokoine Mbeya, akageuza kauli.
    Manyika aliposti picha katika pozi la kimahaba na Naima kwenye akaunti yake ya Instagram akiambatanisha na ujumbe; “Anayesema mrembo huyu ananiua kiwango aje kudaka yeye, kwa sababu mimi siyo hanithi, nina haki ya kuwa na mpenzi kama watu wengine, mkihisi sifanyi kazi yenu vizuri, mniache,”.
    Kufatia kuenea kwa ujumbe huo, inadaiwa mlinda mlango huyo chipukizi aliitwa na viongozi wa Simba SC jana na matokeo ya kikao chake na mabosi wake yamekuwa kuomba radhi.
    “Wanadamu wengi wanafanya makosa bila kutambua kwa kuwa na upeo mdogo wa kufikiri. Wanachama na viongozi nawaomba radhi kwa kitendo nilichokifanya kijana wenu. Mnisamehe sana, naahidi kutojitokeza tena jambo hili. Nawapenda sana na ninaipenda sana Simba Sports Club. Asanteni,”. 
    Lakini mapema kabla ya hapo, mpenzi wake naye, Naima aliposti picha ya pozi la kimahaba na kipa huyu ikiwa imeambatana na ujumbe; “Nakupenda sana mume wangu,”. 
    Manyika alisajiliwa Simba SC msimu huu kama kipa wa tatu, lakini baada ya kutokea dharula ya makipa wa kwanza, Ivo Mapunda na Hussein Sharrif ‘Casillas’ kuwa majeruhi, akajikuta anaanza kazi mapema Msimbazi.
    Tayari Manyika amekwishaidakia Simba SC mechi 22 za mashindano yote na kufungwa mabao 16, wakati kipa wa pili, Casillas aliyesajiliwa pia msimu huu, amedaka mechi nane tu na kufungwa mabao manne.
    Kipa wa kwanza, Ivo Mapunda aliyesajiliwa Desemba mwaka juzi, hadi sasa amedaka mechi 36 na kufungwa mabao 24. 
    Naima naye ameposti picha na ujumbe wa kudhihirisha upendo wake kwa Manyika Jr.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANYIKA AWAOMBA RADHI SIMBA SC, ASEMA TATIZO NI UPEO MDOGO WA KUFIKIRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top