// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAN CITY WAUWEKA REHANI UBINGWA ENGLAND, WAPIGWA 2-1 SELHURST PARK - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAN CITY WAUWEKA REHANI UBINGWA ENGLAND, WAPIGWA 2-1 SELHURST PARK - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
    Tuesday, April 07, 2015

    MAN CITY WAUWEKA REHANI UBINGWA ENGLAND, WAPIGWA 2-1 SELHURST PARK

    MANCHESTER City wamezidi kupoteza matumaini ya kutetea taji la Ligi Kuu ya England kufuatia kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Crystal Palace Uwanja wa Selhurst Park usiku huu.
    City sasa wanabaki na pointi zao 61, baada ya kucheza mechi 31, wakiwa nyuma ya mahasimu, Manchester United wenye pointi 62, Arsenal 63 na Chelsea 70.   
    Glenn Murray aliifungia bao la kwanza Crystal Palace dakika ya 34 licha yaa kupigiwa kelele za kuotea, kabla ya Jason Puncheon kufunga bao la pili kwa mpira wa adhabu dakika tatu tangu kuanza kipindi cha pili. 
    Jason Puncheon akishangilia baada ya kuifungia bao la pili Crystal Palace
    Shuti la mpira wa adhabu la Jason Puncheon likiupita ukuta wa Man City kuelekea nyavuni

    Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure aliifungia bao la kufutia machozi Man City zikiwa zimebaki dakika 12 mchezo kumalizika.
    Kikosi cha Crystal Palace kilikuwa: Speroni, Ward, Delaney, Dann, Kelly, McArthur, Ledley, Puncheon, Zaha, Bolasie/ Pape Souare dk84 na Murray/ Yaya Sanogo dk83.
    Manchester City; Hart, Sagna, Kompany, Demichelis, Clichy, Navas/Nasri dk77, Fernandinho, Toure, Silva, Dzeko/ Lampard dk66 na Aguero.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN CITY WAUWEKA REHANI UBINGWA ENGLAND, WAPIGWA 2-1 SELHURST PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry