// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MALINZI ‘AMLILIA’ JOHN MASHOEU SHOE ALIYEAGA DUNIA JANA AFRIKA KUSINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MALINZI ‘AMLILIA’ JOHN MASHOEU SHOE ALIYEAGA DUNIA JANA AFRIKA KUSINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, April 22, 2015

    MALINZI ‘AMLILIA’ JOHN MASHOEU SHOE ALIYEAGA DUNIA JANA AFRIKA KUSINI

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Kusini (SAFA) Dk. Danny Jordan kufuatia kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Bafana Bafana, John Lesiba "Shoe" Mashoeu (pichani juu) kilichotokea jana Aprili 21.
    Katika salamau zake kwa Dk. Jordan, Malinzi amesema nchi ya Afrika Kusini imepatwa na pigo kubwa katika tasnia ya mpira wa miguu, kufuatia kifo cha  Mashoeu aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa Kansa ya Utumbo, na  kusema watanzania wako nao pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo.
    John Lesiba "Shoe"  Mashoeu aliyezaliwa Desemba 18, 1965 nchini Afrika Kusini, alikuwa ni miongoni wa wachezaji wa nchi hiyo waliotwaa Ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 1996 nchini Afrika Kusini na baadae kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Ufaransa mwaka 1998.
    Wakati wa uhai wake Mashoe alipata kuvichezea klabu za Giant Blackpool, Kaizer Chiefs, Amazulu na Alexandria United vya Afrika Kusini, na timu Gencleribirligi, Kocaeilispor, Fenerbahce na Busrsapor za Uturuki.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI ‘AMLILIA’ JOHN MASHOEU SHOE ALIYEAGA DUNIA JANA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top