TIMU ya vijana ya Chelsea imewatangulia kaka zao kusherehekea ubingwa- baada ya kuifunga mabao 2-1 Manchester City Uwanja wa Stamford Bridge jana na kutwaa ubingwa wa vijana wa Kombe la FA England.
Chelsea imebeba taji hilo kwa ushindi wa jumla wa 5-2, baada ya awali kuwafunga City 3-1 katika mchezo wa kwanza. Katika Ligi Kuu ya England, Chelsea inaelekea kuivua ubingwa Man City.
City ndiyo walioanza kupata bao kupitia kwa Kelechi Iheanacho dakika ya tano, kabla ya Isaiah Brown kuwasawazishia The Blues dakika 15 baadaye.
Tammy Abraham akafunga bao ake la tatu dhidi ya City katika mechi mbili za Fainali, dakika ya 35 kuwahakikishia taji la Chelsea, ambalo pia walilitwaa mwaka 2012, na wakawa washindi wa pili mwaka 2013.
Mmiliki wa Chelsea, bilionea Mrusi, Roman Abramovic alikuwepo uwanjani kuwashuhudia makinda wa The Blues wakiinua ‘ndoo’ ya vijana ya FA na alikuwa mwenye furaha ya kutosha.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Collins, Aina, Tomori, Clarke-Salter, Dasilva, Colkett, Musonda/Ali dk84, Boga/Palmer dk73, Abraham/Sammut dk68, Solanke na Brown.
Manchester City: Haug, Maffeo, Adarabioyo, Humphreys, Angelino, Bryan, Wood/Garcia dk68, Nemane, Celina, Iheanacho/Buckley dk71 na Barker.
Wachezaji wa Chelsea wakisherehekea taji la FA baada ya kuifunga Manchester City mabao 2-1 katika fainai ya pili jana
PICHA ZAIDI NENDA:
http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3057999/Chelsea-2-1-Manchester-City-agg-5-2-Isaiah-Brown-Tammy-Abraham-target-Blues-seal-FA-Youth-Cup-four-years.html#ixzz3YanYL9Gg
0 comments:
Post a Comment