TIMU ya Liverpool imetupwa nje ya Kombe la FA, baada ya kufungwa mabao 2-1 na Aston Villa katika Nusu Fainali jioni ya leo Uwanja wa Wembley.
Liverpool walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa kiungo wao Philippe Coutinho dakika ya 30, kabla ya Christian Benteke kuisawazishia Villa akimtungua ‘ndugu yake’ Simon Mignolet.
Kiungo wa Aston Villa, Fabian Delph alifunga bao la ushindi dakika ya 54 kuihakikishia timu yake Fainali ya FA.
Kiungo na Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, alichezeshwa kwa mara ya kwanza leo tangu atolewe kwa kadi nyekundu dhidi ya Manchester United, lakini hakutengeneza nafasi ya kuvaa jezi ya Liverpool atakapokuwa akitimiza miaka 35 Uwanja wa Wembley.
Aston Villa sasa itamenyana na mabingwa watetezi wa FA, Arsenal katika fainali ambao jana waliitoa Reading katika muda wa nyongeza kwa 2-1 pia.
Kikosi cha Aston Villa kilikuwa; Given, Bacuna, Vlaar, Baker/Okore dk26, Richardson, Cleverley, Westwood, Delph, N'Zogbia/Sinclair dk75, Benteke, Grealish/Cole dk84.
Liverpool; Mignolet, Can, Skrtel, Lovren, Markovic/Balotelli dk46, Henderson, Allen/Johnson dk78, Coutinho, Moreno/Lambert dk91, Gerrard na Sterling.
Christian Benteke akiruka hewani kushangilia bao lake Uwanja wa Wembley leo
0 comments:
Post a Comment