KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema kwamba anakabiliwa na jukumu la kuisuka upya timu hiyo ili kuwa na kikosi kitakachoweza kuingia nne bora ya Ligi Kuu England hatimaye kucheza Ligi ya Mabingwa.
Matumaini ya Liverpool kwenda Ligi ya Mabingwa yameanza kuyeyuka baada ya kufungwa 1-0 jana na Hull City, kwani sasa timu ya Rodgers inazidiwa pointi saba na wapinzani wao, Manchester United walio nafasi ya nne.
Baada ya kumuuza Luis Suarez msimu uliopita na kushuhudia aliyekuwa pacha wake, Daniel Sturridge akiwa nje muda mrefu msimu huu sababu ya majeruhi, Rodgers amekiri ubora wa Liverpool umeshuka.
Brendan Rodgers amesema anahitaji kuisuka upya Liverpool iweze kucheza tena Ligi ya Mabingwa
Rodgers hapati tena huduma ya Luis Suarez aliyehamia Barcelona msimu huu
"Kwa mashabiki na wachezaji wakati wote ni vizuri kama utapata aina ya wachezaji ambao hakika watakusaidia, mmoja au wawili labda tunahitaji," amesema Rodgers.
"Klabu inahangaika sana na wamiliki watatusapoti katika hilo. Kama wapo na watafaa, klabu itafanya kikla kitu kuwapata. Hiyo ndiyo changamoto ya msimu ujao: kujenga timu ambayo itapita kwenye maji,".
0 comments:
Post a Comment